Don na Maxine Simpson wakiwa hospitalini
Amini Usiamini mapenzi ya kweli bado yapo humu duniani!
Kisa
kimoja ambacho kimedhibitishia wengi baada ya wapenzi wawili waliooana
na kuishi pamoja kwa takriban miaka 62 walipoaga dunia pamoja.
Don
na Maxine Simpson walikuwa wakazi wa mji wa Bakersfield, ulioko jimbo
la California, Marekani waliaga dunia saa nne baada ya kushikana mikono
hospitalini na kuahidiana penzi lao halitafifia kamwe hata mauti
iwapate.
Lakini
punde alipoaga Maxine na mwili wake ukaondolewa chumbani walikokuwa
wamelazwa pamoja na mumewe Don, zilipata saa nne tu uchungu ulipomzidi
Don na akakata roho iliwaendelee kupendana na mkewe ahera.
Mjukuu
wao Melissa Sloan aliiambia runinga ya KERO-TV Kuwa Don alimhusudu sana
nyanya yake yaani Maxine tangu alipomtupia jicho mnamo mwaka wa 1952
walipokutana katika mashindano ya Bowling.
Wapenzi hao wawili waliooana mwak huohuo na hawajawahi kuachana tangu hata katika mauti.
''Babu
yangu alikuwa anatamani kuishi na nyanya yangu na hata baada ya wawili
hao kuanza kuugua kutokana na umri wao mkubwa waliwaomba wasimamizi wa
hospitali walimolazwa wasiwatenge.''
Don alikuwa na miaka 90 huku mke wake akiwa na miaka 87.
Don na Maxine Simpson walipokutana
''Babu
yangu alihudumu kama mwanajeshi katika jeshi la Marekani naye bibi
alikuwa ni muuguzi haswa walipokuwa huko Ujerumani ambapo waliwahi
kuishi kwa muda mrefu.''alisema mjukuu wao Melissa.
Wamemuacha nyuma mtoto mmoja wa kiume na wajukuu watano.
No comments:
Post a Comment