Wananchi wakipita kwenye dimbwi la maji maeneo ya Posta Mpya jijini Dar es Salaam jana asubuhi baada ya kujaa maji.
Eneo
hilo ambalo lipo mkabala na Benki ya Posta kwa muda mrefu zimekuwa
likijaa maji kutokana na mitaro ya Barabara ya Azikiwe kuziba lakini
wahusika ambao ni Halmashauri ya Manispaa Ilala inaonesha wameshindwa
kulimaliza hivyo kuleta usumbufu kwa watu wanatumia barabara hiyo pamoja
na magari.
Maji yakiwa yameeneo katikaeneo hilo karibu na kituo cha kuuzia mafuta.
Kijana akipita kwenye dimbwi hilo mbele ya maegesho ya Tax katika eneo hilo.
Mwendesha baiskeli ya magurudumu matatu akipita eneo hilo.
Wazungu waamua kutembea peku
Licha
ya kuwepo kwa madimbwi ya maji yaliyochanganyikana na maji taka
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam , raia hao
wa kigeni ambao hawakufahamika wanatoka taifa gani walinaswa na kamera
ya mtandao wa habari za jamii.com wakipita maeneo ya posta mpya jirani
na jengo la IPS wakiwa pekupeku jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.
Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja walikokuwa wakienda.
Kwa
miaka ya hivi karibuni kumekuwa na baadhi ya madhehebu kutoka nje ya
nchi ambayo waumini wake hawavai viatu kutokana na imani zao.
No comments:
Post a Comment