10157122_791481054226467_2516584315463168131_n
Hili ndio tukio lililosababisha kufukuzwa kazi wakiwa na sare za kazi.
Na Mwandishi wetu, Kagera
Jeshi la× Mkoa wa Kagera, limewafukuza kazi askari watatu wa× Kikosi cha Usalama barabarani ‘Trafiki’ kwa kukosa la kupiga picha zisizo na maadili wakiwa na sare za kazi.
Picha hiyo ilianza kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii hivi karibuni zikionyesha askari hao wakiwa katika ‘mahaba’ huku wamevaa sare za× Jeshi hilo.
Akitoa taarifa mbele ya wandishi wa habari mapema jana Oktoba 9, mkoani Kagera,  Kamanda wa× Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe, na kuthibitisha kufukuzwa kazi askari hao.
Kamanda Mwaibambe, alieleza kuwa askari wawili na mwenzao aliyewapiga picha, wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi kwa kitendo hicho cha kulidhalilisha× Jeshi la Polisi.
10351371_293561717508395_306800HGIK086339793833_n (1)
Picha za askari hao na askari huyo wa kike akiwa kwenye mavazi ya kawaida.
Kamanda Mwaibambe, aliwataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788, PC Fadhili Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme, wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani× Misenyi, mkoani humo.
Mwaibambe, alisema kuwa askari hao walitenda kosa hilo mwaka 2012 wakiwa kazini.
Alisema, PC Fadhili ndiye aliyehusika kupiga picha hizo kwa kutumia simu yake ya kiganjani na kuanza kuzituma katika mitandao ya kijamii, akijua kuwa kitendo hicho ni kinyume cha maadili.
Kamanda Mwaibambe, alitaja sababu za kuwafukuza kazi askari hao kuwa ni kupiga picha tatanishi na kuzituma katika mitandao wakati wakijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume na maadili ya× Jeshi hilo.
Aidha, Kamanda Mwaibambe alikiri kuwa picha hizo sio za kutengeneza bali ni halisi, na kuwataka askari kufahamu na kuheshimu maadili ya× Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi hilo.
1524763_293473614183872_7088304712953395660_n (1)