Hali ya Rais Kikwete yazidi kuhimarika,awasiliana na wananchi kwa simu yake ya mkononi
Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete akiwasiliana na baadhi ya wananchi waliokuwa wakimjulia
hali kupitia simu yake ya mkononi kupitia ujumbe mfupi(sms) .Rais
Kikwete anayepata matibabu katika hospitali ya Johns Hopkins jijini
Baltimore Maryland nchini Marekani anaendelea vizuri na anafanya mazoezi
mara kwa mara na afya yake inaendelea kuimarika(picha na Freddy Maro)
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete juzi, Jumatatu,
Novemba 10, 2014, alianza kuwasiliana na mamia kwa mamia ya wananchi
mbali mbali nchini kujibu ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wa kumpa pole,
kumtakia heri na nafuu ya haraka ambao amekuwa anatumiwa na wananchi
tokea mwishoni mwa wiki.
Tangu alipofanyiwa
upasuaji wa tezi dume (prostrate) Jumamosi iliyopita kwenye Hospitali ya
Johns Hopkins, Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, Rais Kikwete
amepokea mamia kwa mamia ya SMS zikimpa pole na kumtakia nafuu ya
haraka.
Rais Kikwete bado
anaendelea kujibu SMS hizo na wananchi ambao wamemtumia SMS Rais Kikwete
waendelee kusubiri majibu ya Mhe. Rais kwa sababu anakusudia kujibu SMS
zote ambazo ametumiwa.
Aidha, Rais Kikwete
jana alizungumza kwa simu na uongozi wa juu wa Tanzania kwa mara ya
kwanza tokea afanyiwe upasuaji. Rais alizungumza na Makamu wa Rais
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt.
Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda.
Wakati huo huo,
madaktari wanaondelea kumtibu Rais Kikwete jana waliondoa bandeji kwenye
sehemu ambako alifanyiwa upasuaji wakieleza kuwa hali yake inaendelea
vizuri na anapata nafuu kwa kasi nzuri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete juzi, Jumatatu, Novemba 10, 2014, alianza kuwasiliana na mamia kwa mamia ya wananchi mbali mbali nchini kujibu ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wa kumpa pole, kumtakia heri na nafuu ya haraka ambao amekuwa anatumiwa na wananchi tokea mwishoni mwa wiki.