ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, December 1, 2014

BASI LAACHA NJIA NA KUTUMBUKIA KORONGONI MLIMA KITONGA

 Basi liitwalo Easy Bus  lenye namba za usajili T 298 BLZ lililokuwa likitokea Lilongwe Malawi likiwa katika mtaro wa Mlima Kitonga.



Foleni kubwa iliyosababishwa na basi hilo baada ya kuingia mtaroni na kuziba njia.
 Basi la abiria lenye namba za usajili T 298 BLZ likiwa linatolewa katika mtaro wa Mlima Kitonga mapema leo baada ya kutumbukia.
 Hali hii imesababisha foleni kubwa kwa magari huku mengine yakishindwa kuendelea na safari zake. Kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha gari hilo kutumbukia mtaroni ni kufuatia kupata hitilafu na hatimaye uamuzi wa kuliegesha kando ukafanyika kisha abiria wote wakashuka ili kusubiri marekebisho hayo.
Haikupita muda mrefu baada ya abiria kushuka gari lilikosa balansi, likaanza kurudi kinyumenyume na kisha kuingia mtaroni. Hakuna mtu aliyefariki dunia wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...