"Hongera kwa
ushupavu uliouonyesha...", Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaonekana
kumwambia kijana Kassim Saidi Kassim wakati wa kupiga picha ya pamoja,
baada ya kumtunuku Nishani ya Ushupavu Ikulu jijini Dar es salaam.
Wengine katika picha ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi
na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete
akimvisha Nishani ya Ushupavu Kassim Said Kassim ambaye ni muuza Chips
katika maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam, Kassim alitunukiwa
Nishani hiyo baada ya kupambana na jambazi aliyevamia na na kupora wateja
katika eneo la biashara yake na kumpiga chepe na kusababisha kupatikana
kwa bastola moja pamoja na risasi tano.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete juzi, Jumanne, Desemba 9, 2014 ametunuku Nishani ya Ushupavu kwa
mfanyabiashara ya kukaanga na kuuza viazi (chips) wa Dar es Salaam ,
Bwana Kassim Saidi Kassim, kwa kitendo chake cha kuokoa wananchi dhidi
ya jambazi.
Bwana Kassim Saidi
Kassim alikuwa mmoja wa watunukiwa 28 wa nishani mbali mbali ambazo Rais
Kikwete alitunuku ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Miaka 53
ya Uhuru.
Katika sherehe ya kutunuku nishani iliyofanyika kwenye Bustani za Ikulu
Katika sherehe ya kutunuku nishani iliyofanyika kwenye Bustani za Ikulu
Rais Kikwete alieleza
kuwa amemtunuku Bwana Kassim Nishani hiyo kwa sababu ya kitendo cha
ushupavu alichokionyesha cha kujitoa mhanga kukabiliana na jambazi
mwenye silaha ambaye angeleta madhara makubwa.
Katika maelezo
yaliyosomwa kabla ya Rais Kikwete kumtunuku Nishani hiyo, ilielezwa kuwa
mnamo Julai 7, mwaka jana, 2013, majira ya saa 3:15 usiku, Bwana Kassim
akiwa katika eneo lake la biashara, alitokea jambazi akiwa na silaha
aina ya bastola na kuanza kuwashambulia wateja kwa kuwapiga makofi na
kuwapora mali zao na fedha zao.
Iliendeleza
kuelezwa: “Kwa ushupavu mkubwa ulichukua chepe na kumpiga jambazi huyo
mara mbili kichwani, kipigo kilichosababisha aanguke na kupoteza fahamu.
Kitendo hicho kilifanikisha kukamatwa kwa bastola aina ya Glock ambayo
nambari zake zilikuwa zimefutwa ikiwa na risasi tano ndani yake na hivyo
kuepusha madhara ambayo yangeweza kusababishwa na matumizi mabaya ya
silaha hiyo.”
Bwana Kassim anakuwa
muuza chips wa kwanza katika historia ya Tanzania kutunukiwa Nishani ya
Ushapavu na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bwana Kassim mwenye umri wa miaka 28 alizaliwa katika Kijiji cha Namwinyu, Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma mwaka 1986.
Alisoma na kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 2002 katika Shule ya Msingi ya Ilala, iliyoko Wilaya ya Ilala, Dar Es Salaam.
Baada ya kumaliza
elimu ya msingi, alianza kujishughulisha na biashara ya kukaaga na kuuza
viazi (chips) katika eneo la Buguruni Malapa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Desemba,2014
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Desemba,2014
No comments:
Post a Comment