Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova
akifurahi jambo wakati akizungumza na Askari Polisi waliomaliza Mafunzo
ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika vyuo vya Polisi vya Moshi na
Zanzibar,wakati alipowapokea leo Desemba 4,2014 katika Kituo cha Kati
cha Polisi,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Askari
Polisi waliomaliza Mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika
vyuo vya Polisi vya Moshi na Zanzibar wakimsikiliza Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova,wakati
akiwaasa maswala mbali mbali yahusuyo Jeshi hilo.
Kamishna wa Polisi
Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam amewapokea askari waliomaliza
mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika vyuo vya Polisi vya
Moshi na Zanzibar ambao ni utaratibu wa kawaida na kuwaasa mambo
yafuatayo:
• Amewataka
kutumia ujuzi na maarifa walivyopata katika mafunzo yao ili kuondoa
kero za uhalifu katika jiji la Dar es Salaam. “Matukio ambayo ni kero
katika jiji la Dar es Salaam ni pamoja na matumizi ya Dawa za kulevya,
ujambazi wa kutumia silaha, na kero nyingine, madanguro, grocery
katikati ya barabara, na muziki unaopigwa kiholela katika makazi ya
watu”. Alisema Kamishna Kova.
• Aliwataka
washirikiane na askari wenzao katika oparesheni inayoendelea jijini Dar
es Salaam kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba ili kuthibiti vitendo vya
uhalifu ambavyo kwa kawaida hujitokeza kwa wingi katika kipindi hicho.
• Aidha,
wahitimu hao wametakiwa kusimamia na kudumisha nidhamu katika Jeshi la
Polisi ili kuwafanya wananchi wapate huduma nzuri pamoja na kuleta
taswira nzuri ya Jeshi la Polisi.
• Amewaasa
askari hao kufuata maadili ya kazi ya Polisi na kufanya kazi kwa bidii
na maarifa kwani wanaweza kupata vyeo vya juu, kuwa mfano na wakawa
viongozi bora Jeshini.
Mwisho amewataka
kushirikiana na wananchi katika mitaa mbalimbali na kufanya doria ili
kila mtaa jijini Dar es Salaam uwe huru dhidi ya uhalifu.
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.



No comments:
Post a Comment