Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Baada ya kuchapwa mabao 2-0 na mahasimu wao wa soka Simba SC katika mchezo wa ‘ Hisani Nani Mtani Jembe’ siku ya Jumamosi iliyopita, klabu ya Yanga SC imeamua kufikia maamuzi magumu ya kumfuta kazi kocha Marcio Maximo na ni wazi Mholanzi, Hans Van De Pluijm atachukua nafasi hiyo. Hii ni mara ya pili kwa Yanga kumfukuza kazi kocha wao mara baada ya kufungwa na Simba. Ikumbukwe mwaka uliopita, Mholanzi, Ernie Brandts aliondoshwa baada ya kufungwa mabao 3-1 katika Mtani Jembe.Tofauti na ilivyokuwa kwa Brandts ambaye aliifundisha Yanga kwa mwaka mmoja na kuisaidia kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/13, Maximo yeye amefukuzwa baada ya kuiongoza timu hiyo katika michezo tisa ndani ya miezi mitatu. Yanga imepoteza michezo miwili kati ya saba ya ligi kuu msimu huu, Maximo ambaye alianza vizuri klabuni hapo kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii, alipoteza mchezo wa kwanza tu wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Kocha Van Der Pruijm akiwa na Shaffih Dauda mara tu baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere
Kocha wa zamani wa Yanga mdachi Hans Van Der Pruijm amesema amerudi tena kwenye timu yake ya zamani kuendeleza pale alipoishia,
‘Falsafa yangu ipo
pale pale ya kucheza soka la kushambulia, kwasababu naamini ili ushinde
mchezo ni lazima ufunge mabao ya kutosha’.
Van Der Pruijm akifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Clouds TV mara tu baada ya kutua usiku wa saa nane na nusu usiku.
Kocha huyo amesema bado hajasaini mkataba ila ana matumaini makubwa atamalizana na wakurugenzi wa klabu pale watakapokutana,
Van Pruijm anakuja kuziba pengo la kocha aliyetimuliwa Mbrazil Marcio Maximo .
Yanga imeshinda
michezo minne msimu huu, lakini hadi l,igi inasimama katika raundi ya
saba hakuna mtu alikuwa na shaka kuhusu uwezo wa Maximo. Kocha huyo wa
zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amechokwa haraka sana
na mashabiki, wapenzi, wanachama na viongozi wa klabu yake kutokana na
kiwango kidogo cha uchezaji. Mifumo yake ya ufundishaji imekosa mvuto,
lakini kitendo cha kufungwa kidhaifu na Simba kimeshindwa kuvumilika.
COUTINHO, JAJA, EMERSON WAMPONZA?
Ndiyo sababu kubwa,
ukitoa mbinu zake, Maximo alikuwa akiwakumbatia zaidi wachezaji raia wa
Brazil, Andrey Coutinho, Geilson Santos ( ambaye aliomba mwenyewe
kuachwa baada ya michezo saba), kwa Emerson Oliveira siwezi kuzungumzia
kwa sababu mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo alicheza katika kiwango cha
kawaida wakati alipoichezea Yanga kwa mara ya kwanza.
Jaja alifunga mara
mbili dhidi ya Azam, ila alikosa makali katika ligi kuu kiasi cha
kufunga bao moja tu katika michezo saba ya ligi kuu. Alishindwa kumudu
presha ya mashabiki wa Yanga ambao hawakuwa wakipendezwa na kiwango
chake huku uchezaji wake wa taratibu ukiwaboa wengi. Maximo aliwanyima
nafasi washambuaji kama Said Bahanunzi, Jerry Tegete, Saimon Msuva,
Hussein Javu na Hamis Kizza hata pale wachezaji hao wa Kibrazil
waliposhindwa kufanya vizuri.
Kuwang’ang’ania
wachezaji hao na kuwanyima nafasi wale wenye uwezo kumewakera . Brandts
aliondolewa baada ya kufungwa 3-1 licha ya kusaini mkataba mpya wa miaka
miwili zaidi, yeye aliondolewa kwa kuwa alipingana na uamuzi wa
viongozi kuwasajili baadhi ya wachezaji ambao hakuwataka wakati ule.
Brandts ndiye mwalimu
aliyeifanya Yanga kucheza mchezo mzuri wa kupasiana na ndiye
aliyeimarisha kiwango cha wachezaji kama, Saimon Msuva, Frank Domayo (
yuko Azam FC kwa sasa), Juma Abdul, Oscar Joshua na wengineo lakini kwa
Maximo imekuwa ni tofauti, wachezaji wengi wameshuka viwango na
ameshindwa kuwaimarisha wachezaji ambao ‘ wanasua-sua’. Yanga wamefanya
uamuzi sahihi kwa kumuondoa Maximo na Coutinho.CHANZO SHAFIH DAUDA
No comments:
Post a Comment