Kwa mujibu wa ripoti ya World Giving Index 2014, Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye watu wenye roho mbaya barani Afrika.
Hiyo ni kwa mujibu wa
utafiti uliodhaminiwa na Charities Aid Foundation (CAF) na kufanywa na
kampuni ya utafiti ya Gallup na kuhusisha nchi 135 duniani kote. Data
hizo zilikusanywa kuanzia mwaka 2013.
Tanzania ilikamata
nafasi ya 14 kati ya nchi 24 zilizofanyiwa utafiti na kukamata nafasi ya
87 duniani ikiwa na asilimia 27 nyuma ya Kenya ambayo imekamata nafasi
ya kwanza Afrika na nafasi ya 15 duniani ikiwa na maana kuwa ina watu
wakarimu na wanajitolea zaidi kusaidia.
Nchini zenye watu wenye roho mbaya zaidi ni Tunisia, Misri na Congo.
Utafiti huo ulifanywa kwa kuwauliza washiriki kama wamewahi kufanya mambo haya:
Wamechanga fedha
kwenye charity yoyote, wamejitolea kusaidia taasisi yoyote, kumsaidia
mtu asiyemfahamu au kumsaidia wasiyemfahamu baada ya kumuomba msaada.
Marekani imeongoza kwenye orodha hiyo.

No comments:
Post a Comment