ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Tuesday, December 16, 2014

Watoto 134 ni kati ya watu 141 waliouwawa na Taliban huko Pakistan







 Wanafunzi walionusurika
Takriban watu 141 wakiwemo wanafunzi 134 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya wapiganaji wa Taliban kuvamia shule moja inayosimamiwa na jeshi huko Peshawar kaskazini - magharibi mwa Pakistan.
Wakuu wa Hospitali wanasema kuwa zaidi ya watu 40 wanasemekana kujeruhiwa japo idadi hiyo inatarajiwa kupanda zaidi.
Maafisa mjini Peshawar wanasema kuwa wanaume watano ama sita waliokuwa na silaha waliingia shuleni hapo wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi .
 Wanafunzi mia tano na waalimu walikuwa katika shule hiyo ya umma ya kijeshi wakati shambulizi hilo lilipotokea .
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa walisikia milio ya bunduki iliyodumu kwa dakika kadhaa .
Wanasema pia kuwa walisikia sauti za kelele za wanafunzi na waalimu .
Wanajeshi wakijiandaa kwa makabiliano na wapiganaji wa Taleban
Haijabainika wazi ni kwa namna gani wanamgambo wa Talebain waliweza kupenya hadi kuingia ndani ya majengo hayo yanayomilikiwa na jeshi.


Jeshi la Pakistan limesema operesheni ya uokozi ilikuwa ikiendelea na kwamba wengi wa wanafunzi na waalim wameokolewa toka eneo la hatari.

Shambulio hilo limetokea wakati operesheni kubwa ya kijeshi ikiendelea dhidi ya wapiganaji wa Taleban wa Pakistan na wanamgambo wengine wanaoendesha harakati zao kaskazini mwa jimbo la Waziristan.chanzo Bbc

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...