CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha, kimesema hakina mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, aliyeandaliwa hadi sasa.
Kimesema
mgombea mwenye sifa za kulikomboa jimbo hilo, ambalo liko Chadema,
hajajitokeza mpaka sasa. Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili hivi
karibuni, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Arusha ,Feruzi Banno alisema chama
kina utaratibu wake wa kampeni na chama hakina mgombea aliyeandaliwa kwa
kuwa muda wa kuandaa wagombea bado haujatangazwa.
Banno
alisema hayo alipotakiwa na gazeti hili, kufafanua kauli zilizozagaa
jijini Arusha kuwa chama hicho kimemwandaa mmoja wa wagombea (jina
tunalo) ambaye yuko mstari wa mbele kulitaka jimbo hilo kwa udi na
uvumba na tayari ameanza harakati za kampeni kwa kushirikiana na baadhi
ya viongozi wa CCM kata, wilaya na mkoa.
Alisema
taarifa hizo zimekuwa zikisambazwa na wana CCM wenye kutaka ubunge Jimbo
la Arusha, ambao wanaoana kama wanatengwa. Alisema kura za maoni za
kumsaka mgombea ubunge ndani ya chama, ndizo zitakazoamua na si
vinginevyo na kamwe chama hakitambeba mwana CCM .
Pamoja na
hayo yote, Katibu huyo alisema Jimbo la Arusha lenye asilimia kuwa ya
vijana, linahita mgombea mwenye kujichanganya katika rika zote na
anayekubalika bila ya kubabaisha,kwani huyo atafanya chama kufanya kazi
kwa urahisi na sio ngumu katika kampeni.
Banno
alisema kuwa CCM inahamu ya kulikomboa Jimbo la Arusha Mjini hivyo
hatuhitaji mgombea mzigo, ambaye itafika siku ya mwisho tukaanza
kulaumiana hilo halitakubalika kamwe kwa uongozi wa chama wilaya.
‘’Tunataka mgombea kijana, mwenye kujichanganya katika vijiwe mbalimbali
vya Jiji la Arusha na mwenye kujulikana katika kila kona ya Jimbo la
Arusha na mgombea huyo bado hajajitokeza hadharani.
Hiyo
itasaidia chama kufanya kazi ndogo sana lakina hatutaki mgombea ambaye
chama kitafanya kazi ya ziada kumnadi, hilo halitakubalika kamwe. ‘’
Baadhi ya wana CCM waliojitokeza na kuonesha nia ya kuwania ubunge Jimbo
la Arusha Mjini ni Kamanda wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa
wa Arusha , Philemon Mollel na Wakili wa Kujitegemea, Victor Njau.
Mwingine ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa, Dk Arod Adamson na Deo Mtui. CHANZO:HABARI LEO
No comments:
Post a Comment