Nimeona nijitokeze hadharanio kwa kumpongeza sana Mh Zitto.kwa namna ambavyo amepambana dhidi ya wakorofi Wakenya huko twitter
Kwamba,alipost kuhuji juu ya maamuzi ya marufuku iliyotolewa na waziri
wa uhusiano wa Africa Mashariki na utalii wa Kenya juu ya marufuku ya
kuingia magari ya Tanzania nchini Kenya
1.Ghafla,akadakia
na kupost waziri wa utalii Kenya na kusema serikali ipo sahihi na
kuonyesha dharau juu ya watanzania,kwa kusema hakujafanyika mkutano
wowote na anahitaji makubaliano ya mwaka 198
Kwamba,wadau mablimbali nikiwepo mie tukampa moyo Zitto kwa kusema
hakuna haja ya dialogue,huko ni kuwabembeleza,kinachotakiwa tuwazuie
baadhi ya bidhaa zao kuingia kwetu,ndio tuzungumze
2.Kwamba,Zitto akapost na kusema kuwa kama waziri atoe marufuku
hiyo.kama la, nasi tuweke marufuku Maziwa kutoka Kenya yasiuzwe Tanzania
na kwamba''Rais wao Kenyatta aondoke na Maziwa yake"
3.Mara akadakia Seneta sharobaro Mike Sonko,akapost na kusema kuwa
atakuja TZ ili kusisitiza Zitto kumuomba radhi Rais
Uhuru(nitamkaribisha) kwakuwa ni mwenyekiti wa EAC.kwa maneno ya
".....aondoke na maziwa yake"
4,Zitto akapost na akasema .Tena inapaswa Zitto na Bunge zima la Tanzania liombe radhi rais Uhuru
Rai Yangu
- Kwa sasa wakenya chini ya Seneta Sonko wameanzisha kampeni ya kumchafua Mh.Zitto na Tanzania mtandaoni kwa kutuonyesha hatufai kwa lolote kwao
- Watanzania wote inapaswa kumuunga mkono Zitto kwa hili,na kupambana na hao wakenya ambao wameanza chokochoko za mitandaoni
- Inawezekana wamechoka kuwa na hili shirikisho la Afrika Mashariki?
- Karibu sana Seneta Sonko tukufundishe diplomasia ya Usharobaro ulioenda Shule.Msamaha?kwa Lipi?

No comments:
Post a Comment