
Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Dk Shein

Makamu wa kwanza wa Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad
Mustakabali
wa uhai wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), upo shakani
kutokana na wananchi kutofautiana kuhusu umuhimu wa kuendelea na mfumo
huo wa uongozi, huku baadhi wakitaka iitishwe Kura ya Maoni kuamua hatma
ya serikali hiyo.
SUK
iliundwa mwaka 2010 baada ya vyama vikuu vya siasa visiwani hapa, CCM na
CUF, kujadiliana na hatimaye kufikia muafaka wa kugawana madaraka ili
kuondoa siasa za chuki zilizotokana na machafuko ya mwaka 2005 wakati
wananchi walipokuwa wakipinga matokeo ya Uchaguzi wa Rais.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti la Mwananchi unaonyesha kuwa iwapo Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) haitakuwa makini katika usimamiaji wa kanuni
na sheria za uendeshaji wa kampeni hadi kuelekea Uchaguzi Mkuu, kuna
uwezekano mkubwa wa wanasiasa wa pande mbili kuyatumia vibaya majukwaa
na kuiparaganyisha serikali hiyo.
Tatizo
jingine linaloonekana kuinyemelea SUK ni kuibuka kwa watu wanaotaka
ifanyike Kura ya Maoni na wananchi kuulizwa kama wanataka mfumo huo wa
uendeshaji serikali kwa pamoja unastahili kuendelea.
Kutoimarika
kwa huduma za jamii chini ya SUK kama ilivyotegemewa na wananchi na
malengo yake kutofikiwa kunaelezwa pia kuwa ni kati ya changamoto
zinazoikabili SUK.(P.T)
Akizungumza
na Mwananchi, mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Asasi za
Kiraia Zanzibar (Angoza), Mohamed Hafidh Khalfan alitetea SUK akisema
kwamba faida zimeonekana, ikiwamo kudumishwa kwa amani na kuondoa
mgawanyiko katika jamii, lakini akasema yapo mambo yanayohitaji
kufanyiwa marekebisho ya msingi kulinda ustawi wa serikali hiyo.
Khalfan
alisema viongozi wa juu wa SUK bado wanaona kwamba mfumo huo wa
uendeshaji Serikali ni miliki yao binafsi isiyohusisha wananchi. "Ndani
ya mwaka mmoja, wananchi walitakiwa kupewa elimu ya uraia kuhusu SUK kwa
kuzishirikisha asasi za kiraia; Serikali imewaacha wananchi
wakigawanyika na kuwa na ufahamu mdogo wa mfumo wenyewe.
Hili ni
tatizo linalotishia uhai na mustakabali wa jambo hilo," alisema Khalfan.
Pia alisema kuwa kwa miaka minne, SUK imeshindwa kuleta na kuibua
mabadiliko ya msingi serikalini kutokana na makatibu wakuu, makamishna,
wakuu wa mikoa na wilaya kubaki watu wale wale huku wakiteuliwa kwa
kuangaliwa itikadi zao kisiasa na kushindwa kusukuma uwajibikaji na
utendaji wenye tija.
Kamishna
mstaafu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Simai Mohamed Said alieleza
kuwa bado SUK ina umuhimu mkubwa licha ya kujitokeza baadhi ya watu
kuipinga bila ya kuwa na nguvu ya hoja na kutojali kuhesabu mema
yaliyopatikana, huku wakitoa kasoro haba zinazoweza kufanyiwa
marekebisho ya msingi.
Simai alisema uhai wa SUK umetokana na hekima, uongozi bora na siasa safi ya Dk Shein katika kusimamia Serikali kisera.
Alisema
zipo faida lukuki zilizopatikana tangu kuundwa kwa mfumo huo, ikiwa ni
pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar bila kujali itikadi
zao za kisasa, kuikosoa serikali kila inapoteleza au kujisahau.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Serikali Zanzibar (Suza), Ali Haji Vuai alisema
malengo ya SUK kimsingi yalikuwa matatu, moja ikiwa ni kuondoa hofu ya
kisiasa.
Vuai
anasema SUK imeishia katika hatua moja kati ya hizo, ambayo aliitaja
kuwa ni kuiunganisha jamii kutokana na chuki za kisiasa, lakini akakosoa
ujenzi na utendaji wa uendeshaji serikali hiyo, akisema bado
haujabadilika kutokana na nyadhifa nyingi za watendaji wakuu kunufaisha
upande mmoja.
Alisema
kosa kubwa ni kukosekana kwa imani ya pamoja na badala yake vyama viwili
vinaunda Serikali moja ambayo inatekeleza sera ya chama kimoja.
No comments:
Post a Comment