Magari ya jeshi la Chad yaliyotumwa Cameroon kupambana dhidi ya Boko Haram.
Shambulio
hili limefanyika usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii katika mji
wa Ngouboua kando ya Ziwa Chad. Washambuliaji walisafiri eneo hilo
wakitumia mitumbwi mitatu.
Watu
kadhaa wameuawa akiwemo mkuu wa kijiji. Baada ya shambulio hilo, jeshi
la Chad liliingilia kati na kuwatimua wanamgambo hao wa Boko Haram.
Kundi la
Boko Haram, limeendesha shambulio hilo usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa
wiki hii katika kijiji cha Ngouboua pembezoni mwa ziwa Chad, kilomita
mbili na Nigeria, ambapo wanamgambo wa kundi hilo waliingia katika
kijiji hicho wakitumia mitumbwi mitatu.(P.T)
Wauaji
hao walijigawa katika makundi mawili. Kundi la kwanza liliendesha
shambulio dhidi ya ngome ya vikosi vya usalama, wakati ambapo kundi la
pili lilikua likichoma mota shemu moja ya kijiji hicho cha Ngouboua, na
kusababisha hofu miongoni mwa wakazi. Katika mapiagano hayo na vikosi
vya usalama vya Chad, mwanajeshi mmoja ameuawa na wengine wanne
wamejeruhiwa, kulingana na idadi iliyotolewa na jeshi la Chad. Upande wa
raia wa kawaida, mkuu wa kijiji cha Ngouboua ameuawa na wakazi wengine
watatu wamejeruhiwa.
Jeshi la
Chad lililazimika kutumia ndege za kivita. Jeshi la Chad limebaini
kwamba ndege zake za kivita zimeshambulia kwa mabomu mitambwi mitatu
ambayo walikitumia katika usafiri kwa kuingia katika kijiji cha
Ngouboua. Idadi ya wanajeshi na askari wa polisi imeongezwa katika
kijiji hicho. Hata hivyo operesheni ya kuwasaka wanamgambo wa Boko Haram
inaendelea.
No comments:
Post a Comment