
Mmoja wa washiriki wakiuliza maswali katika warsha hiyo
Kimela Bila Mwandaaji wa Kipindi cha Walinde Watoto akizungumza katika Warsha hiyo
Mathias
Haule, Afisa Maendeleo ya Jamii maswala ya Ukatili dhidi ya Watoto
kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akielezea Sheria
ya Mtoto
Neema Kimaro, Mratibu wa kipindi cha Walinde Watoto kutoka True Vision Production akiendelea na maandalizi ya warsha
Rose Minja, Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya familia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,
akijibu maswali ya washiriki wa Warsha inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili
dhidi ya Watoto nchini Tanzania
Washiriki wa Warsha inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania
Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ushirikiano na UNICEF
wameandaa warsha ya siku tatu inayohusu nafasi ya vyombo vya habari
katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania.
Warsha hiyo inayofanyika mjini Moshi inashirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wawakilishi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Wawakilishi kutoka wilaya za Hai na Moshi Manispaa, wawakilishi kutoka UNICEF pamoja na wawakilishi wa redio 14 zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.
Wengine ni wawakilishi kutoka Baraza la Habari Tanzania, mwakilishi kutoka Csema pamoja na waandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto kampuni ya True Vision Production.
Warsha hiyo inayofanyika mjini Moshi inashirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wawakilishi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Wawakilishi kutoka wilaya za Hai na Moshi Manispaa, wawakilishi kutoka UNICEF pamoja na wawakilishi wa redio 14 zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.
Wengine ni wawakilishi kutoka Baraza la Habari Tanzania, mwakilishi kutoka Csema pamoja na waandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto kampuni ya True Vision Production.
Akifungua
warsha hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Kilimanjaro, Paul
Shayo alilishukuru shirika la Watoto Duniani (UNICEF) kwa kazi nzuri
ambazo wamekuwa wakizifanya kwa kushirikiana na Serikali katika
kuhakikisha kuwa Haki za Watoto zinatekelezwa hapa nchini.
Paul
alitaja aina za ukiukwaji wa haki za mtoto hapa nchini kuwa ni pamoja
na kuolewa katika umri mdogo, kutumikishwa katika mashamba na ukatili
dhidi ya watoto. Hata hivyo aliendelea kuzitaja athari mbalimbali
zinazotokana na ukiukwaji wa haki hizo kuwa ni pamoja na
watoto kukatishwa masomo na kukosa haki ya kuendelezwa na kwamba ndoa za
utotoni zina madhara kiafya hasa wanapopata ujauzito na kujifungua
katika umri mdogo.
Paul
alimalizia kwa kutoa rai kwa washiriki wa warsha hiyo na kuwataka
wakawe chachu ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto katika maeneo waliyotoka
na kushirikiana na wadau waliopo katika ngazi za vijijini, mikoani na
mijini kadri inavyowezekana ili kuwalinda watoto na kutokomeza ukatili
dhidi ya watoto.
Vipindi
vya Walinde Watoto vinarushwa na redio 14 ambazo ni Radio Jamii Kilosa,
Country FM, Boma Hai FM, Radio Quran, ZBC pamoja na Redio Kitulo.Nyingine
ni TBC Taifa, Bomba FM, Faraja FM, Uplands FM, Ice Fm, Radio Maria,
Radio Kwizera na Zenj FM. Vipindi hivi vinapatikana pia katika tovuti
ya www.walindewatoto.org na kupitia www.facebook.com/WalindeWatoto
No comments:
Post a Comment