MSAMA
Promotion kwa mara nyingine tena imeandaa Tamasha kubwa la nyimbo za
kumsifu Mungu litakalofanyika wakati wa sikukuu ya Pasaka katika mikoa
tofauti hapa nchini.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama anasema kwamba
tamasha hilo mwaka huu litakuwa na utofauti mkubwa ukilinganisha na
matamasha mengine yaliyopita, kwani limeboreshwa zaidi na watakuwa
wanafurahia miaka 15 tangu lianzishwe.
"Kwanza
kabisa tofauti na matamasha yaliyopita, mwaka huu tutakuwa na waimbaji
wengi zaidi wa muziki wa Injili kutoka nchi za nje.
"Kutakuwa
na waimbiaji kutoka Kenya, Zambia, Afrika Kusini, Rwanda, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC) na nje ya Afrika, ambapo lengo kubwa ni
kulifanya tamasha hili kuwa na utofauti," anasema.
Moja ya
maboresho makuwa katika miaka 15 ya Tamasha la Pasaka la mwaka huu Msama
amesema kwamba litakuwa na kiingilio rahisi zaidi ili kila mmoja aweze
kuhudhuria na kupata baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu.
"Waimbaji
wote maafuru wa muziki wa Injili watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri
mno kuhakiksha kwamba tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali," anasema.
Anasema
kutokana na ukumbwa na maboresho mazuri zaidi ya tamasha hilo, kamati ya
maandalizi imewashirikisha watu 100, wakiwa ni wachungaji na
Wainjilisti.
Anasema
lengo kubwa la kuwashirikisha wachungaji na Wainjilisti ni kwa sababu
watu wengi waweze kubarikiwa kiroho kwa kuwa tamasha hilo ni la kumsifu
Mungu.
"Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi kwani watashiba kiroho kutokana na kuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho.
"Tutaheshimu
mno maoni ya wapenzi wa tamasha hili kutoka sehemu mbalimbali na kila
watakalotushauri tutalifanyia kazi, lengo kubwa lilikuwa n kiboresha
tamasha letu," anasema.
Mwaka huu
Tamasha la Pasaka linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni
ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam na limekuwa likijiongezea
umaarufu na kukubalika zaidi kutokana na ubunifu wake wa kufanya
maadhimisho ya Sikukuu za Pasaka na Krismasi kwa umahiri na mguso wa
kiroho kupitia matamasha hayo.
Umaarufu
wa matamasha hayo pamoja na mambo mengine, unatokana na ukweli kuwa
yamekuwa yakifanyika kwa ubunifu na umakini mkubwa huku kila mwaka
yakiongezeka na kubadili waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa
ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya
nyota waliowahi kutumbuiza katika matamasha hayo ni marehemu Angela
Chibalonza kutoka Kenya, ambaye naye aliwahi kutikisa.Baadhi ya nyimbo
zake zilizotikisa na kukonga nyoyo ni Yahwe Uhimidiwe na Uliniumba
Nikuabudu.
Wengine
walioweka historia nchini ni pamoja na Solly Mahlangu kutoka Afrika
Kusini. Mwimbaji huyo alivunja rekodi ya waimbaji wote licha ya kuwa
hafahamu lugha ya Kiswahili vilivyo, lakini aliweza kuimba nyimbo kadhaa
za Kiswahili kama Mwambamwamba ili kwenda sawa na Watanzania aliokonga
nyoyo zao kwa kuwapa neno la Mungu kupitia muziki wa Injili.
Sipho
Makhabane, Rebeka Malope nao kwa nyakati tofauti, walifanya vizuri
ukiachilia mbali waimbaji wengine kama Ephraim Sekeleti kutoka Zambia,
Ambassadors of Christ (Rwanda), Faraja Ntaboba na Solomoni Mukubwa
(Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), 24 Elders (Uganda) na Anastazia
Mukabwa (Kenya).
Rebecca
amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009),
Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at
Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits
(Januari 10, 2006).
Kwa
upande wa Mukubwa ambate ametamba sana na wimbo wa Mfalme wa Amani
amepata kutamba katika tamasha hilo na albamu mbalimbali ikiwemo ya
Usikate Tamaa yenye nyimbo kama Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke
Si Nguo, Usikate Tamaa, Moyo Tukuza Bwana, Chunga Ahadi Yako na Yesu
Jina Zuri.Pia ana albamu nyingine mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na
Mungu Mwenye Nguvu.Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya
kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu,
Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio.
Albamu yake ya pili ya Mungu Mwenye Nguvu ina nyimbo za Mungu Mwenye
Nguvu, Mkono wa Bwana, Mfalme wa Amani, Siku Moja, Tabia Ina Dawa na
Roho Yangu Ikuimbie.
Pia yupo
msanii, Solly Mahlangu 'Obrigado' wa Afrika Kusini ambaye ingawa
alitumbuiza Tamasha la Krismasi, lakini amekuwa na mvuto mkubwa kwa
mashabiki.
Mahlangu
ni muimbaji ambaye anashika kasi katika anga ya muziki wa Injili Afrika
ambaye pia anamudu kuimba Kiswahili kizuri kwa baadhi ya nyimbo zake.
Mbali ya
kuwa maarufu katika nyimbo za Iinjili nchini mwake, pia ni Mchungaji
ambaye ana uwezo wa kufanikisha muziki wa Injili na kanisa lake ambalo
ni Word Praise Christian Centre Intenational lililoko Tembisa.
No comments:
Post a Comment