
Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnuye akikutana na Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe alipofika katika Ofisi za Free Media, wachapishaji wa
gazeti la Tanzania Daima, leo akiwa katika ziara katika vyombo vya
habari ambayo aliianza jana, jijini Dar es Salaam.

Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana kwa furaha na Mhariri
Mtendaji wa Free Media, Nevile Meena alipowasili kwenye kampuni hiyo leo
akiwa katika ziara kwenye vyombo vya habari mjini Dar es Salaam

Nape
akizungumza na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Free Media wachapishaji
wa gazeti la Tanzania Daima leo jijini Dar es Salaam

Nape
akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za gazeti la Jambo
Leo, leo mjini Dar es Salaam, akiwa katika ziara hiyo. Wapili kushoto ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concept inayochapisha gazeti hilo,
Teophil Makunga.

Nape
akiagana na mpigapicha mkuu wa Jambo Leo Richard Mwaikenda mwishoni mwa
ziara katika chumba cha habari cha magazeti hayo. Picha na Bashir
Nkoromo na Adam Mzee

Nape akiwa kwenye chumba cha Breaking news cha magazeti ya Jambo Leo

Baadhi ya waandishi wa habari katika chumba cha habari cha magazeti ya Jambo Leo

Nape akimkabidhi zawadi ya kalenda ya CCM, Makunga
No comments:
Post a Comment