Wema Sepetu akiwasha gari Jipya la ASX Mitsubishi katika uzinduzi wa gari hilo jijini Dar es Salaam.
Hili ndilo gari la ASX Mitsubish jipya lililozinduliwa hivi karibuni katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.(P.T)
Na Mwandishi wetu Dar es Salaam
Mtangazaji
wa Clouds FM, Millard Ayo na mwigizaji maarufu nchini, Wema Sepetu
wamesifia gari jipya la Mitsubishi ASX la mwaka 2015 linalouzwa na
kusambazwa na kampuni ya Diamond Motors (Hansa Group).
Katika uzinduzi wa kutambulisha gari hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine Kampuni ya Diamond Motors wauzaji pekee wa magari kutoka Mitsubishi waliwaalika Millard Ayo na Wema Sepetu kujaribu gari hilo toleo jipya Mitsubishi ASX kabla ya uzinduzi.

Mastaa
hao walivutiwa na mwonekano wa Mitsubishi ASX lenye vioo vya kisasa juu
vyenye mwanga unaomwezesha dereva na abiria kufurahia mwonekano wa pande
zote.
Meneja
mauzo wa Diamond Motors, Reena Ganatra alisema Gari hilo lenye luninga
ndogo inayocheza DVD, iPods, Bluetooth na sauti kutoka vyanzo mbalimbali
ni maalumu kwa vijana wa kisasa na familia kwani Mitsubish ASX
limetengenezwa na teknolojia ya MIVEC yenye kulifanya liwe na nguvu ya
150 ps katika 6,000 rpm na nguvu ya kuzunguka kwa mwendokasi mkubwa na
kwamba limetengenezwa maalum kutumia mafuta kidogo.
“ASX ni
mwanzo tu, tunazo aina nyingine za magari kama kama Pajero ambayo
tunakaribia kuyatambulisha sokoni ili kuwapatia watanzania magari imara
na yenye kuaminika kutoka Mitsubishi” Alisema Ganatra.
ASX toleo la 2015 limebuniwa kwa ubora wa hali ya juu na imara likiwa na bodi gumu pia lina mfumo maalumu usiotegemea funguo hivyo kumfanya mwendeshaji kuwasha injini kwa kubofya kitufe.
ASX toleo la 2015 limebuniwa kwa ubora wa hali ya juu na imara likiwa na bodi gumu pia lina mfumo maalumu usiotegemea funguo hivyo kumfanya mwendeshaji kuwasha injini kwa kubofya kitufe.
“ASX
kutoka Mitsubishi, imetengenezwa maalumu kukidhi mazingira ya Tanzania
hasa mijini kama Dar es Salaam ambapo muda wowote dereva wa kawaida
anatoka kwenye barabara nzuri na kuingia kwenye barabara zenye
makorongo” alisema Ganatra
Injini ya
gari hilo ambayo ni 2.0-liter imeunganishwa INVECS-III CVT inayoisaidia
mwendelezo wake katika kubadili mwendo pamoja na uimara wa usukani
unaosaidia mikono ya dereva kuwa salama hata anapokuwa katika mwendo
mkali.
Hansa
Group inayofanya biashara kama Diamond Motors Limited, imekuwa ikifanya
kazi ya katika sekta ya usafirishaji tangu mwaka 1980, ikitoa huduma kwa
wasambazaji na wadau wa usafiri.Kampuni hiyo huhusika na bidhaa/ huduma
mbalimabali. Shughuli za Hansa Group zimesambaa karibu nchi zote za
jumuia ya Africa ikitoa huduma kama vile za uchimbaji, Umeme, Mafuta na
Gesi, Reli,Ulinzi, Ujenzi, Usafiri, kimataifa na jumuhia za kimataifa.
No comments:
Post a Comment