
Mtoto
Baraka Cosmas Rusambo mwenye umri wa miaka sita mwenye ulemavu wa ngozi
(Albinism), amekatwa mkono wa kulia katika tukio lilitokea Jumamosi
usiku tarehe7 Machi kwenye kijiji cha Kiseta, wilayani Sumbawanga
vijijini, mkoani Rukwa.
Matukio
ya ukatili dhidi ya albino yanaendelea kuwa tishio nchini Tanzania baada
ya mtoto wa miaka sita kukatwa kiganja cha mkono
Shambulio hilop jipya limetokea mkoani Rukwa kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Mtoto huyo kiume Baraka Cosmas alikuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao walipovamia nyumba yao.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Rukwa Jackob Mwaruanda amesema kwa sasa mtoto huyo
anapata matibabu hospitali na hali yake inaendelea vizuri.
Polisi inaendelea na uchunguzi kubaini wahusika.
Shambulio
hilo linajitokeza wiki moja tu baada ya watuhumiwa wanne kuhukumiwa
adhabu ya kifo kwa mauaji ya albino, Na muda mfupi baada ya Rais Jakaya
Kikwete kukemea mauaji ya albino, ambao viungo vyao hutumika katika
shughuli za kishirikina kwa imani potofu kuwa zinasaidia kuleta utajiri
na mad.(P.T)
No comments:
Post a Comment