Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli akikagua ujenzi wa kituo cha
Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) Morocco jijini Dar es Salaam siku
za hivi karibuni. Picha na Maktaba
Na Ibrahim Yamola, Mwananchi
Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya CAG katika
kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa
iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013
kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa
sahihi.
“Hizi ni fedha kwa ajili ya Counterpart fund,”
alimkariri Lukuvi ambaye sasa ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.
Chanzo cha habari kimeeleza kuwa ripoti ya CAG
imeeleza kuwa, “Katika kikao cha kuanza ukaguzi huo Aprili 3, mwaka jana
uongozi wa wizara ulithibitisha kwamba hakukuwa na barabara mpya bali
walifanya hivyo baada ya kuona madeni yamekuwa makubwa kiasi cha Sh420
bilioni kama yalivyokuwa kwenye hesabu za wakala wa barabara za mwaka wa
fedha 2010/11.”
Katika ukaguzi huo imebainishwa kuwa Sh3 bilioni hazikujulikana matumizi yake.
Taarifa zaidi zinasema baada ya wizara kupeleka
fedha kwa wakala wa barabara, fedha hizo zilifanyiwa mchakato wa
kuzigawa upya lakini nyaraka halisi zilizotumika kugawa fedha hizo
hazikuwasilishwa kwa ukaguzi.
“Hata hivyo, kati ya Sh175.3 bilioni zilizopitia
kwenye akaunti ya maendeleo ya wakala wa barabara, kiasi cha
Sh3,048,365,229 hakikuweza kupatiwa maelezo jinsi kilivyotumika.
“Pia, kati ya malipo ya Sh77.7 bilioni
yaliyofanyika kwa wakandarasi au washauri wa barabara moja kwa moja
kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Novemba 30, mwaka 2011 kupitia
barua ya kumbukumbu namba GA.65/263/01/VOL.XI Gavana Mkuu wa BoT,
alikanusha kulipa asilimia 30 ya fedha hizo Sh30.6 bilioni.
“Gavana wa BoT amekanusha kulipa Sh30.6 bilioni
kwa kampuni ya M/S Strabag Internationl Gmbn na M/S China-Engineering
Corporation Co, kati ya Sh77.7 ambacho kilipelekwa BoT kwa ajili ya
malipo kwa wakandarasi au washauri mbalimbali,” alifafanua zaidi mtoa
habari hizi na kuongeza:
“Ukaguzi maalumu umeshindwa kuthibitisha malipo
yenye jumla ya Sh47.1 bilioni sawa na asilimia 61 kama yalilipwa kwa
walengwa waliokusudiwa kwa sababu Gavana wa BoT amesema kuwa kisheria
hatakiwi kutoa taarifa za wateja.”
Pia, habari za ndani kutoka ofisi ya CAG zinadai
kuwa, Sh13.4 bilioni za ujenzi wa barabara za mikoa zilitumika kulipia
barabara binafsi na za halmashauri za wilaya ambazo hutengewa fedha
kupitia mfuko wa barabara kinyume na makusudio yaliyopitishwa na Bunge.
“Pia, nimebaini kwamba baadhi ya miradi haikuwamo
kwenye kasma zilizopitishwa na Bunge kwenye makisio ya mwaka wa fedha
2010/11 na miradi mingine ilitengewa fedha kidogo lakini wakala wa
barabara alitumia fedha nyingi kulipia miradi hiyo bila kuonyesha jinsi
alivyozipata,” chanzo cha habari kimekariri ripoti ya CAG.
Katika ukaguzi huo, ufisadi mwingine wa Sh36.6
bilioni ambazo ni malipo ambayo hayakutolewa taarifa kwenye ripoti za
washauri au wakandarasi, jambo linaweza kuwapo kwa uwezekano mkubwa wa
wakandarasi kuidai Serikali zaidi ya mara moja na kuitia Serikali
hasara.
Mtoa habari wetu alisema kuwa Sh6.2 bilioni
zilitumika kuwalipa wakandarasi ambao hawakuonyeshwa katika orodha ya
madeni yaliyowasilishwa bungeni pamoja na malipo ya Sh6.6 bilioni
yaliyokwishalipwa yaliombewa tena.
No comments:
Post a Comment