Timu ya
Young Africans maarufu kama Yanga ndiyo timu pekee ya Tanzania
iliyobakia katika michuano ya Shirikisho la Kandanda barani Afrika, CAF
kwa mwaka 2015.
Yanga wameweza kusonga mbele kwa kuwaondoa BDF XI ya Botswana kwa kuwacharaza jumla ya mabao 3-2.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijiji Dar es Salaam, Tanzania, wiki mbili zilizopita Yanga waliwafunga BDF XI magoli 2-0
Timu hizi ziliporudiana mjini Gaborone, Botswana, Ijumaa usiku, BDF XI waliibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Hata hivyo ushindi huo haukuwasaidia kwani walijikuta wanatolewa katika mashindano kwa kufungwa jumla ya mabao 3-2.
Sasa Yanga itacheza na timu ya FC Platinum ya Zimbabwe katika hatua inayofuata. FC Platinum iliitoa Sofapaka ya Kenya.
Timu ya
Azam iliyopata ushindi mzuri wa mabao 2-0 dhidi ya El Mereikh ya Sudan,
katika kinyang'anyiro cha klabu bingwa barani Afrika ilijikuta ikipoteza
mchezo wa marudiano mjini Khartoum baada ya kulazwa mabao 3-0 na hivyo
El Mereikh kufuzu kwa jumla ya mabao 3-2.
Timu
nyingine za Tanzania Zanzibar za KMKM na Polisi zimejikuta zikitupwa nje
ya michuano ya vilabu barani Afrika kwa kupoteza michezo yao.CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment