ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Diamond. Show all posts
Showing posts with label Diamond. Show all posts

Wednesday, January 21, 2015

Diamond Apelekwa Polisi na Wema


MKALI wa filamu nchini na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu ‘Wema’, amemfungulia kesi ya madai mpenzi wake wa zamani ambaye ni mwanamuziki wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, kwa kumtapeli kiasi cha Sh milioni 10.
Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la Utangazaji (BBC) idhaa ya Kiswahili, Wema aliripoti madai yake kituo cha Polisi Oysterbay akidai kuwa alimpatia mwanamuziki huyo kiasi hicho kwa makubaliano ya kazi na kuahidi kumlipa, lakini amekwenda kinyume makubaliano yao.
Muhusika mkuu ambaye ni Wema alitoa maelezo kwamba watu wanamtupia lawama kutokana na hatua aliyofikia, lakini amedai kuwa amelazimika kufanya hivyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeingia dhamana na taasisi Focus Vicoba kuchukua fedha hizo.
“Naona watu wengi wananilaumu kwa kuwa nimemfungulia kesi Diamond, pasipo kuelewa kama fedha hizo pia hazikua zangu bali ni mkopo ambao niliingia dhamana katika taasisi ya utoaji mikopo ya Vicoba.
“Kupitia mfuko wa Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la kumpatia Diamond, ili aweze kuandaa miradi yake tena kwa makubaliano kuwa atazirudisha ili tuweze kufanya marejesho ya mkopo tuliochukua,” alisema Wema.
Mrembo huyo alieleza muda waliiopeana ahadi ya kurudisha fedha hizo umepita na Diamond haoneshi dalili ya kuzirejesha wakati wanatakiwa kuzirudisha kwa wakati .
“Yote haya yasingenikuta, lakini sina jinsi kwani natakiwa kurudisha pesa za watu nimekuwa nikimpigia simu Diamond hataki kupokea simu zangu, lakini kama alitaka kunidhulumu ni bora angejiunga mwenyewe na hawa Vicoba ili apate mkopo na kufanya mambo yake au kama aliona hawezi kwa kujishtukia basi angetumia ile tovuti yao, angepata kwa urahisi na hakuna mtu yeyote angejua kama amekopa ila sio kukimbia kulipa deni la watu,” alisema.
Hata hivyo Diamond ambae kwa sasa yupo nchini Burundi kwa ajili ya ziara yake kimuziki, tayari ametumiwa taarifa na jeshi la polisi kwa barua ya wito kufika kituoni pindi atakaporejea nchini, huku mama yake mzazi akifikishiwa ujumbe huo nyumbani kwake.
Wema ambae alimwekea dhamana, yupo katika kipindi kigumu ambacho kinaweza kupelekea kufilisiwa mali zake ambazo aliziandikisha wakati wa kuchukua mkopo huo ili ziweze kufidia deni hilo.
Kwa mujibu wa kiongozi wa taasisi hiyo ambae aligoma kutajwa jina lake gazetini, alisema kuwa ni kweli Wema alifika katika ofisi zao zilizopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ili apewe muongozo lakini alipotakiwa kufuata taratibu za kiofisi kama wanachama wengine wanavyofanya katika vikundi, hakukubaliana na utaratibu, hivyo kushauriwa ajiunge kupitia tovuti .
MTANZANIA ilimtafuta Meneja wa Wema, Martin Kadinda, ambae alieleza hajui chochote kuhusu kufungulia kwa kesi hiyo, akaomba apewe muda kumtafuta msanii huyo ili aweze kupata ufafanuzi juu ya suala hilo, lakini hakueleza nini kilichojiri na kusisitiza asubiriwe.
Gazeti hili halikuishia hapo, lilimsaka Meneja wa Diamond, Babu Tale, ambae alionekana kushtushwa na habari hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote.

Saturday, September 20, 2014

PICHA ZA WANANDOA WAPYA,DADA WA DIAMOND,ESMA NA PETIT MAN


 Ni habri mpya ya mjini kwa sasa,ndoa ya Dada 
wa Diamond na kipenzi wa Wema petiti man wakuache
,amabapo uhusiano wao ulioanza kama utani hatimae  umezalisha kile amabcho wengi
 hawakukitgemea kama kingekuwa mapema hivi...
Tunawatakia maisha mema ya ndoa na barka tele








Monday, September 1, 2014

DIAMOND ADAIWA KUOKOLEWA NA POLISI WA UJERUMANI,KUFUATIA MASHABIKI WAKE KUSHIKWA NA HASIRA

 Gari ya Polisi ilioibuka kumuokoa Diambond kufuatia sakata la mashabiki wake kupandwa na jazba
Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini stuttgart,ujerumani


UJERUMANI SI SHWARI KIMENUKA !!

POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA ! KASHINDWA KUWIKA STUTTGART KISA ?

KAFIKA UKUMBINI SAA 10 ALFAJIRI ! WASHABIKI WANASURI SHOW TANGU SAA 4 USIKU

PROMOTA MNAIJERIA AINGIA MITINI ,DJ APATA KISAGO HETI VYOMBO VIBOVU ! HAIBU

Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muzikima-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.

Mmoja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la haibu alijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwawanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Thursday, May 22, 2014

“AJ UBAO” & DIRTY HERRY To Perform Alongside Diamond Platnumz In Houston Texas This Memorial May 25 !


dmk
BRAND NEW HITS FROM AJ & DIRTY HERRY ON THE STAGE WITH WCB 
#WE SUPPORT OUR TALENTS#ENT WILL BE TELEVISED ON THE RED CARPET#
GET YOUR TICKETS NOW WWW.DIAMONDUSATOUR.COM

Wednesday, February 5, 2014

HUYU NDIYE MLINZI BINAFSI WA SUPER STAR DIAMOND PLATZNUM CHECK HERE MAHERA YA AJABU ANAYOLIPWA KILA WIKI





Mlinzi wa Binafsi wa Super Star Diamond Platznum maarufu kama mwarabu analipwa Shillingi Laki Tano kila Wiki, ni mwenye fulana nyeusi mwanzo hapo!!

Thursday, November 21, 2013

Video ya "MY NUMBER ONE" ya Diamond yaanza kurushwa kwenye channels kubwa kubwa duniani.


d8
Lilikuwa swali kwamba inakuaje video iliyotumia ya gharama kubwa zaidi ya msanii wa bongoflava haipati airtime kwenye vituo vya kimataifa wakati video nyingine za wasanii wa muziki huu huu wanafanikiwa kupata airtime.
Jibu la swali hilo hatimaye limepatikana baada ya video ya My number one kuanza kuchezwa kwenye vituo maarufu duniani.
Diamond kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii aliwajulisha mashabiki wake kwamba wanaweza pia kuiona video ya My number one kwenye channel ya Trace na Sound City.
Kupitia Trace video hiyo imetambulishwa kama video mpya na kwenye Sound city imerushwa kwenye trending video request na hizi ni picha kutoka kwenye screen wakati video hiyo ikipata airtime kwa mara ya kwanza kwenye vituo hivi.

d1
d2
d3
d6
d7


Friday, October 4, 2013

UNIQUE BIRTHDAY YA DIAMOND


 Kila mtu anaithamini na kuipenda tarehe ya siku 
yake ya kuzaliwa,ni siku ambayo baadhi yetu huifurahia kwa
 mitindo tofauti tofauti kulingamna 

Tuesday, September 3, 2013

AUDIO:SIKILIZA MSANII MASANJA MKANDAMIZAJI AKIFUNGUKA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA NA SERIKALI KUSHIKILIA PASSPORT YAKE



Masanja Mkandamizaji afunguka alipolonga na Vijimambo kuhusu kudaiwa kuhusika na madawa ya kulevya na kuhusu kushikiliwa kwa Passport yake na Serikali, MSIKILIZE

Hii ndio Nyumba ya Ghorofa ya Masanja Mkandamizaji inayomhusisha na madawa ya kulevya

Friday, July 12, 2013

PREZZO AMPONDA DIAMOND


Majigambo ya Diamond kwenye vyombo vya habari kabla ya Tamasha la Matumaini kufanyika kuhusu kumgalagaza Prezzo kwenye show hiyo hayajampendeza Rapcellency na sasa ameamua kujibu.

Prezzo ambaye jina lake halisi ni Jackson Makini alianza kwa kuweka picha ya gazeti inayowaonesha akiwa na Diamond kwenye habari iliyohusu tamasha hilo na kuandika ‘Hahahaha #DomoSeriously????
Rapper huyo hakuishia hapo aliweka picha nyingine ya Diamond na kuandika: “U talkin money or u talkin nonsense au anashindana na ndovu kun***a?

Mwisho alimalizia kwa kujibu tweet ya mtu mmoja aliyemwambia kuwa huyo ni Diamond kwa kuandika: Unfortunately only “diamonds” I know is the ones on ma neck fam.”
 
Mashabiki walimjia juu sana prezoo kama inavyoonekana hapa chini:




Msanni Prezzo wa Kenya atakuwa amepata sample ya majibu ya baadhi ya fans wake ambao wengi ni wakenya baada ya kumdiss Diamond Platinumz wa Tanzania kupitia akaunti yake ya twitter July 10.


Sample ya majibu hayo inaweza kuonekana kupitia comments zote za fans kwenye habari iliyowekwa na mtandao wa ghafla wa nchini Kenya, ambapo asilimia 99 wameonesha kutokubaliana na alichokifanya.



Edwin Mwashegwa : ah, Diamond achana na huyu mbulula, wewe unda hela!, bifu za ki***ge hazifai.



Top Commenter: Prezzo umepita hiyo age ya beef za kishenzi. Ingia studio utoe kitu, otherwise kwa musiki diamond ako juu. I feel you bro! anything to remain relevant and grab some headlines.



Bellah Ongachi : aaarggh Diamond is waaayy better.. n am sure by the time he hits the years prezzo has stayed in the entertainment scene he'll be miles ahead..so your thing diamond.



Caroline Karijo : Mhhhhh who even listens to to him Jaguar and Diamond r much better than him n we all knw,,,,,,, he can continue playing women who stoops low for him.



Yvonne De Cole : Prezzo ni wivu nini,,,, leave the highest paid musician in East Africa alone,,, ana mulla en he is still simple doesn floss,,,, prezzo inherits yet flosses



De Sheriff : Diamond, silence is the best weapon. let the baby throw tantrums. Prezzo, its tym to mature up.



Diamond hadi sasa bado hajazungumza chochote.

Wednesday, June 19, 2013

DIAMOND AAHIDI KUMFUNIKA VIBAYA PREZZO SHOO YA USIKU WA MATUMAINI 2013

Diamond akilonga na Sauda kuhusu shoo kali atakayotoa Usiku wa Matumaini 2013.
Sauda na Diamond wakiwa mbele ya kamera.
Platnumz akijiaandaa kabla ya mahojiano.
...Akibadilishana mawazo na Sauda kabla ya kuanza mahojiano.
Mtu wa kamera akiwa mzigoni.
---
Na Wilbert Molandi
MKALI wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ametamba kufanya shoo kali ikiwemo kumfunika msanii wa Uganda, Prezzo katika Tamasha la Matumaini 2013 litakalofanyika Sikukuu ya Sabasaba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.Diamond ametoa majigambo hayo wakati wa mahojiano na Mtangazaji wa kituo cha Star TV, Sauda Mwilima.

“Nimeahidi kufanya bonge la shoo kwenye Tamasha la Matumaini siku hiyo, mashabiki wangu na wapenzi wa muziki wajitokeze kwa wingi.“Ninataka kudhihirisha ubora wangu siku hiyo kwa kumfunika vibaya Prezzo,” alisema Diamond.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...