ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Edward Ngoyay Lowassa. Show all posts
Showing posts with label Edward Ngoyay Lowassa. Show all posts

Friday, December 13, 2013

Lowassa anusurika kifo katika ajali ya ndege

1441502_490297281087923_1876414922_n
PUBLIC NOTICE – OFFICIAL STATEMENT
  
precision air
Precision Air Flight 422, a flight from Dar es Salaam to Arusha, using ATR 42-600 (code number PWI) departed Dar es Salaam without incident at 11:20am today, 13 December 2013, carrying 37passenger on board. Upon landing in Arusha the aircraft experienced tyre deflation.
All 37 passengers and 4 crews on board are safe.
Due to this, several flights have been impacted and arrangements have been made to re-route some of our flights to uplift our passengers to their various destinations as planned. All direct flights to and from Arusha have been re-routed to Kilimanjaro as per below table due to space constraints in accommodating two ATRs at once at Arusha Airport.
Abiria kadhaa akiwemo aliyekua Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa leo December 13 wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Arusha mchana mchana huu.
Ndege hiyo ni mali ya shirika la ndege la Precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua Arusha.ambapo Matairi yote manne ya nyuma yalipasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria.
Jumla ya watu 41 waliokua kwenye ndege hiy, ikiwa ni abiria 39 na wafanyakazi 4 wametoka salama

Thursday, November 14, 2013

Lowassa: Tuliohuzunika, tutashinda pamoja

lowassapx a10b6
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema waliofurahi na kuhuzunika naye pia watashinda pamoja naye.
Bila kufafanua kauli yake jana, Lowassa aliwaambia wakazi wa Monduli mkoani Arusha kuwa: "Kumbukeni kaulimbiu yangu wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, tulifurahi pamoja, tulihuzunika pamoja na tutashinda pamoja".(HD)
Mbunge huyo wa Monduli alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi mbili za ghorofa za wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli.
Katika hotuba yake fupi, pia alitamba kwamba atayashinda majaribu. Hata hivyo, hakufafanua majaribu hayo... "Kuna vita kubwa, lakini ambacho naweza kusema ni kuwa nayaweza yote kwa yeye anitiaye nguvu."
Kuhusu afya yake ambayo mara kadhaa imeelezwa kuwa siyo imara, kiongozi huyo alisema kwa sasa ni nzuri na imeimarika kupita kipindi kingine chochote.
Lowassa alisema kuanza ujenzi wa majengo hayo ambayo ni utekelezaji wa ahadi zake, ni moja ya ushindi na kuwataka wakazi wa Monduli, kumshukuru Mungu kwa yanayotokea.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole aliwataka wakazi wa Monduli, kumshukuru Mungu kwa kuwa na mbunge Lowassa ambaye anapendwa nchi nzima.
"Monduli Mungu awape nini, Lowassa anaitwa kila mahala kusaidia kutokana na moyo wake wa huruma na hapa ametekeleza ilani yote ya uchaguzi," alisema.
Kauli ya Lowassa imekuja siku chache tangu mtangulizi wake katika nafasi ya Waziri Mkuu, Frederick Sumaye alipomtuhumu hadharani kwamba amekuwa akimhujumu na kumwekea vikwazo vya kisiasa kwa kutumia mbinu chafu. Miongoni mwa mambo yaliyoonekana kumkera Sumaye ni habari iliyoandikwa na gazeti hili Septemba 16, mwaka huu inayohusu mradi wa maji Ziwa Victoria, ambayo Lowassa alinukuliwa akisema kuwa wakati akiwa Waziri wa Maji, aliungwa mkono na mawaziri watatu tu alipopendekeza mradi huo wa maji.
Sumaye alisema: "Najua mhusika ametumia sana mradi huu kisiasa na sisi wengine tumenyamaza japo ukweli tunaujua. Amenilazimisha niseme ukweli kuhusu mradi huu kwa sababu mimi nilikuwa Waziri Mkuu na mradi umetekelezwa chini ya uangalizi wangu," alisema na kuongeza:
"Kama waziri anaweza kubuni na kutekeleza mradi mkubwa hivyo peke yake, sasa akiwa Waziri Mkuu si maji yangefika Dodoma? Mbona hata bado kuna sehemu za Kanda ya Ziwa bado kuna shida ya maji?"
Tangu Sumaye atoe tuhuma hizo ambazo zinahusishwa na vita ya kuwania urais wa 2015, Lowassa hakuwahi kujibu chochote wala kusikika akizungumza hadharani, hadi jana.Lowassa alisema mafanikio yaliyopatikana katika jimbo lake na mengine nchini, yanatokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, ambao umefanywa na Rais Jakaya Kikwete.
"Hakuna kipindi ambacho ilani ya uchaguzi imetekelezwa kwa kiasi kikubwa kama kipindi cha Rais Kikwete naomba sote tumpongeze," alisema Lowassa.
Alisema hivi karibuni amekutana na Rais Kikwete ambaye ametoa Sh3 bilioni za ujenzi wa mabwawa 10 katika wilaya hiyo ili kukabiliana na tatizo la maji.
Wodi hizo za kisasa zinajengwa na Kampuni za Meelo Constraction na Bulem Constraction za Arusha kwa gharama ya Sh1.9 bilioni na zitakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 140 wakati mmoja.
1

Monday, September 16, 2013

LOWASSA ASIMIKWA KUWA CHIFU WA UNYENYEMBE MKOANI TABORA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akivishwa vazi maalum la Kichifu pamoja na kukabidhiwa mkuki na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa Chifu wa Kabila hilo, wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki miaka 124 iliyopita. Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya, mkoani Tabora.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira wakishirikiana kuweka jiwe la msingi katika eneo litakalojengwa mnara wa kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki miaka 124 iliyopita.
 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira wakiwa kwenye picha ya pamoja na machifu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini walioshiriki kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki miaka 124 iliyopita.

Wednesday, June 26, 2013

WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE ZA KATA MPAKA VYUO VIKUU WATOA SHUKRANI ZAO KWA WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASSA


 Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa akisalimiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDOM waliotoka shule za  sekondari za kata, wakati walipofika nyumbani kwake mkoani Dodoma kutoa  shukrani zao kwa hatua waliyofikia kielimu.
  Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye hafla hiyo Juni 25, 2013
Mh. Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha DODOMA, maarufu kama UDOM, ambao walifika hapo wakitokea zile shule za makabwela (Shule za Kata), wamemtaka Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa, achukue fomu za kugombea urais 2015 muda utakapowadia.

Pia wameahidi kujichangisha fedha kwa ajili ya malipo ya fomu hizo endapo italazimika. Kauli hiyo ya kwanza kutoka kwa makundi na watu wasiokuwemo ndani ya siasa, ilitolewa Jumatatu usiku nyumbani kwa Lowasa  mjini Dodoma, wakati kundi la wanafunzi hao walipofika kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia ikiwa ni matunda ya shule hizo, ambazo muasisi wake ni mbunge huyo wa Monduli.
“Mimi ninayofuraha kusimama hapa leo hii, nikiwa mtu tofauti, kwa maana ninayesoma elimu ya juu, baada ya kufanikiwa ,kuendelea na elimu ya sekondari kupitia shule za kata pale Kiluvya Dar es Salaam” anasema Hamida Salum ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza hapo UDOM.

“Wewe ni jembe, kama uliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kwa kipindi kifupi cha miaka 2, ninahakika unaweza kufanya men gi zaidi endapo utakuwa rais wan chi hii” mwanafunzi mwingine wa mwaka wa kwanza, Clementina Ophoro alisema, kwenye salamu za mwanafunzi mmoja mmoja wakati wa utoaji shukrani kwa Lowasa.

Lowasa wakati akiwa waziri mkuu wa Tanzania, kwenye mwanzoni mwa awamu ya n ne ya utawala wa rais Jakaya Kikwete, aliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kote nchini, ili kutoa nafasi zaidi za wanafunzi wa makabwela, walioishindwa kendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa madarasa.
 
Kwa sasa shule hizo zimekuwa zikibezwa na watu mbalimbali kwa maelezo kuwa hazina walimu wa kutosha na uhaba wa vifaa vya kufundishia ikiwemo vyumba vya maabara.

“Mimi ninawashangaa watu wanaosema kuwa eti shule za kata hazifai, kwa vile hazina walimu na vifaa. Haya maneno ni ya kupuuzwa, kwani binadamu hupaswi kukwepa changamoto za maisha” alisema mwanafunzi mwingine Victor Mafuru pia wa mwaka wa kwanza.

Wanafunzi hao wa UDOM waliotoka kwenye shule za sekondari za kata, wameamua kuanzisha umoja wao kote nchini, ili kuendeleza ndoto za kuhakikisha kila mwanafunzi wa mtu masikini anapata elimu.

Kwa kuanzia wanafunzi hao wapatao 600, wameahidi kufundisha bure kwenye shule za umma, wawapo likizo baadaye mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.

Kwa upande wake, Lowasa ambaye alikuwa pamoja na naibu waziri wa kazi na ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba, na mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko Kone, aliwapongeza wanafunzi hao kwa moyo wao wa shukrani na kuwataka wasikatishwe tama na maneno yanayotolewa juu ya ubora wa shule hizo, kwani yeye binafsi anajivunia juhudi zake kupitia sera za chama cha Mapinduzi, zimeweza angalau kutoa wanafunzi wengi kutoka shule hizo kujiunga na vyuo vikuu.

Monday, June 3, 2013

LOWASSA ACHANGISHA 305.4MILLIONI ZA MAENDELEO YA NYASA.



Waziriri Mkuu Mstahafu Mh. Edward Lowassa , akimshuhudia Mke wa Waziri wa Mambo ya Nnje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, Mama Membe wakati akichangia pesa taslimu Tsh.1Millioni wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya Wilaya Mpya ya Nyasa Mkoani Rukwa iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam, ambapo zaidi ya Tsh.305.4Millioni zilichangwa pesa taslim pamoja na ahadi.



Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward L owassa, akipeana mkono na Prof. Mbele akimhamasisha kuchangia pesa wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya Wilaya Mpya ya Nyasa Mkoani Rukwa iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam, ambapo zaidi ya Tsh.305.4Millioni zilichangwa pesa taslim pamoja na ahadi.

Akipeana mkono na Mbunge wa Kibaha Koka Silivestry wakati wa harambee hiyo (aliyekaa katikati) ni Mbunge wa Mbinga Magharibi ambayo imegeuzwa na kuwa Wilaya ya Nyasa.


Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akimkabidhi mchangowake Mratibu wa harambee ya maendeleo ya Wilaya ya Nyasa iliyopo kwenye Mkoa wa Rukwa ambapo yeye na marafikizake walichangia kiasi cha Tsh.65Millioni kwenye harambee iliyokusanyaTsh. 305.4Millioni iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...