ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Kagame. Show all posts
Showing posts with label Kagame. Show all posts

Sunday, January 5, 2014

Upinzani Rwanda wailaumu serikali kwa kifo cha Karegeya

68654D4A-F44A-4749-8ED1-F83CA172B90B w640 r1 s cx0 cy17 cw01 e3899
Viongozi wa vyama vya upinzani Rwanda wanamlaumu Rais Paul Kagame kwa kifo cha mkuu wa zamani wa upelelezi ambaye inaelekea amekabwa kwenye hoteli moja Afrika Kusini.

Wachunguzi wanasema mkuu huyo wa zamani wa usalama Patrick Karegeya alikutwa amekufa katika hoteli moja ya hali ya juu huko Johanesburg.


Akizungumza na Sauti ya Amerika mkuu wa zamani wa jeshi la Rwanda Jenerali Kayumba Nyamwasa amesema kwamba mtu aliyemwita hotelini hapo walikuwa wakifahamiana na alikuwa rafiki yake alipokuwa Rwanda na ni mtu aliyemwamini. Chanzo: voaswahili

Tuesday, November 19, 2013

Kagame, Museveni na Kenyatta washtakiwa Korti ya Jumuiya

kagamepx_deab7.jpg
Serikali za Rwanda, Uganda, Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, zimefunguliwa kesi katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki, zikidaiwa kukiuka mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.
Hatua hiyo inatokana na Serikali hizo kufanya vikao vitatu mfululizo na kuzitenga nchi za Tanzania na Burundi.
Walalamikaji katika kesi hiyo, ni Ally Msangi, David Makata na , John Adam, ambao ni Watanzania, wanaotetewa na wakili Mwandamizi, Jimm Obedi wa jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, walalamikaji wamewaomba majaji katika mahakama hiyo, kutoa tamko la kusitisha utekelezaji wa maazimio yote ya vikao vya wakuu wa nchi hizo tatu.(P.T)
Pia wameomba majaji watoe tamko la kukomesha kurejewa kwa vikao kama hivyo kinyume cha mkataba wa jumuiya hiyo.

Kesi hiyo ya aina yake, ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki na kupokewa na Ofisa Masijala i katika mahakama hiyo, Boniface Ogoti.
Kufunguliwa kwa kesi hiyo, kunakuja siku kadhaa baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzilalamikia nchi hizo, kuhusu kuitenga Tanzania kwa kufanya mikutano mbalimbali ya maendeleo ya nchi zao. Nchi nyingine iliyotengwa ni Burundi.

Kikao cha kwanza cha pamoja kilifanyika Aprili mjini Arusha kabla viongozi hao kukutana Juni 25 na 26 jijini Entebbe nchini Uganda, walidai kuwa na nia moja ya kurahisha mawasiliano katika nchi hizo.
Mkutano mwilingine ulifanyika mjini Kigali Rwanda Oktoba 28 ukiwajumuisha Rais Yoweri Museven wa Uganda, Uhuru Kenyatta (Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini) na Paul Kagame.
Wakili wa walalamikaji Obedi, alisema katika kesi ya msingi, wanawashtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Rwanda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uganda,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

Thursday, August 29, 2013

Rais Yoweri Museven na Rais Kagame wakwepa Bandari ya Dar es Salaam, waenda Mombasa kufungua Gati mpya.




Marais wa Burundi, Uganda na Rwanda, wamehudhuria ufunguzi wa Bandari ya Mombasa, Kenya leo wakipokelewa wenyeji wao Rais Kenyatta na William Rutto!

Kenyatta anasema Mombasa ni 'Gateway of East African Business'. Anadai ni manifesto ya serikali yake kuifanya bandari hiyo kuwa 'busy and friendly port in all over East Africa coastline!'

Endelea kusoma zaidi => http://bit.ly/15gV9Aq

Marais wa Burundi, Uganda na Rwanda, wameudhuria ufunguzi wa bandari ya Mombasa, Kenya leo! Wapo pia na wenyeji wao President Kenyatta na Bwana Rutto! 
Katika matangazo yao, wamesema bandari hiyo itaunganisha Africa kibiashara hasa ikichagizwa na Ujenzi wa barabara Namanga Arusha. Hii inaashiria nini kwa mustabali wa Uchumi wa Tz ambayo 60% ya makusanyo ya kodi yanategemea bandari ya Dsm


 
Museveni kahudhuria kwa kiti chake cha Uenyekiti wa EAC, ndivyo Kagame alivyomtambulisha. Pia Kagame anasema hiyo ndio faida ya Integrated East Africa Community, pia Miundombinu bora ya Bandari ya Mombasa, itaunganisha nchi zote za East Africa.


Kenyata anasema Mombasa ni Gate way of East African Business. Anasema ni manifesto ya serikali yake kuifanya bandari ya Mombasa kuwa busy and friendly port in all over East Africa coastline
Nini hatima ya bandari ya Dsm na siasa zake? Siasa za Kenya hizo wamezindua bandari mpya leo, na wanasema Sudan, Ethiopia na Somalia watatumia bandaria hiyo pia.





Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...