ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label chadema.. Show all posts
Showing posts with label chadema.. Show all posts

Monday, July 15, 2013

Mh. Mbowe afika Polisi Makao Makuu kwa mahojiano





Kwa wale ambao mnakumbuka kuwa siku ya ijumaa usiku wa manane Polisi kutoka Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni wakiongozwa na RCO wa Kinondoni walienda nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba usiku kwa lengo la kumkamata, Mbowe alikuwa safarini na alipitia Airport ya Dsm Hivyo kwenda kwake usiku ni jambo la kushangaza sana , leo amerejea kupitia Airport ya Dar na akaamua kwenda moja kwa moja Polisi ili kujua kulikoni.

Ameambatana na Mawakili wawili, Nyaronyo Kicheere na Peter Kibatala majira ya saa tisa na nusu aliingia Makao Makuu ya Polisi na huko wanaendelea na Majadiliano.

Jambo la kushangaza ni kuwa mahojiano yao yanahusu mambo yafuatayo;

1. Kuwa tamko la Kamati Kuu kuwa Polisi walihusika na mlipuko wa Bomu Arusha... Itakumbukwa alishahojiwa tena na akina Chagonja na mpaka leo hakuna taarifa zozote wazi.
2. Kuwa Polisi wanatumiwa na CCM ndio maana wanaisaidia CCM Katika chaguzi mbalimbali ......na hata bomu la Arusha ilikuwa sehemu ya mkakati huo.
3. Kwamba kauli kuwa JK na Bunge kutokuonyesha dalili zozote za kusikitishwa na hata kushindwa kuhudhuria mazishi ni dalili za serikali kuhusika katika tukio hilo.
source jamii forum

Wednesday, July 10, 2013

TAARIFA ZA KUVAMIWA WAKILI WA MUME WA JOYCE KIRIA, PETER KIBATALA .... UKWELI NI HUU HAPA


Nikiwa na wakili wa Mume Wangu, Peter Kibatala na mwandishi wa habari Makene.

Hivi ndivyo alivyojibu wakili wa mume wangu Henry Kilewo, Wakili msomi Peter Kibatala
Goodmorning:nimepigiwa simu kadhaa toka kwa watu mbalimbali wakinijulia hali baada ya kusoma some post huko Jamii Forum kwamba nimevamiwa,kupigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana kuhusiana na case ninazoendesha kuwatetea Wanaharakati kadha wa kadha.
Nawapa pole wote waliostushwa na taarifa hizi.
Ukweli ni kwamba niko salama,nimerudi jana usiku tokea Tabora nilikoambatana na Joyce Kilewo Kiria.
Nitaendelea kufanya kazi zangu kama wakili kwa maadili ya uwakili bila hofu iwayo yote.Ninasubiri kupangiwa tarehe na Mahakama Kuu kanda ya Tabora kuhusiana na maombi ya marejeo niliyoyawasilisha baada ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora kuwa haina uwezo kutolea maamuzi hoja zetu za kisheria juu ya mashtaka yanayowakabili Henry John Kilewo na wenzake.
Siamini kwamba Tanzania kunaweza kuwa na utaratibu wa kuumiza Mawakili wanaotekeleza majukumu yao ya kisheria.
Post hii naitoa toka Mahakama Kuu Dar es Salaam ninakosubiria kuhudhuria case nyingine kwa mujibu wa majukumu yangu ya kila siku.
Viva Freedom.
Peter Kibatala,
Advocate.

Friday, May 24, 2013

Dr. Slaa sasa anaweza kumuoa Josephine Mushumbusi baada ya kushinda rufani iliyotolewa na mumewe wa zamani

 
Mume wa zamani wa Mushumbusi
 

Katika taabu na raha, katika magonjwa na shida   umpende na kumheshimu siku zote za maisha yako

  Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akiwa na Josephine Mushumbusi
---
HATIMAYE Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na aliyekuwa mume wa Josephine Mushumbusi( KWA  SASA  NI  MCHUMBA WA DR. SLAA) , Maimbo baada ya kuiona rufaa hiyo haina msingi wowote kisheria.
 
Hukumu hiyo ya rufaa ya  madai ya ndoa Na.32/2012 ilitolewa leo na Hakimu Aniseth Wambura ambapo alisema mahakama yake imefikia uamuzi huo wa kuitupa rufaa hiyo kwasababu haina mantiki ya kisheria.
 
Hakimu Wambura alisema mahakama yake imekubalina na hukumu iliyotolewa Aprili 2012 na Mahakama ya Mwanzo Sinza katika kesi ya madai talaka iliyokuwa imefunguliwa na Mushumbusi anayetetewa na wakili wa kujitegemea Philemon Mutakyamilwa  dhidi ya Maimbo ambapo mahakama hiyo ya chini ilitangaza kuwa hakukuwa na ndoa baina ya watu hao kwasababu Maimbo alikuwa ni mzinzi, simwaminifu katika ndoa yake na alikuwa akimtesa mkewe.
 
“Baada ya mahakama yangu kusikiliza hoja za mwomba rufaa na mjibu rufaa ,mahakama hii imefikia uamuzi wa kukubali hoja za Mushumbisi kuwa kwa tabia ile ya mbaya ya uzinzi na ukosefu wa uaminifu katika ndoa yake hapakuwepo na ndoa baina yao hivyo mahakama inatangaza kuwa hukumu ya mahakama ya Mwanzo Sinza ambayo iliivunja ndoa hiyo ilikuwa hukumu sahihi “alisema hakimu Wambura.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili Mutakyamilwa alisema amefurahishwa na hukumu hiyo kwani mahakama imetenda haki  kwasababu kesi hiyo ya madai ya talaka ilikuwa na msukumo wa siasa chafu zilizokuwa na lengo chafu la kumchafulia jina mteja wake(Mshumbusi) ambaye kwa sasa ni mzazi mwenzie Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad Slaa.
 
KWA  HIYO, KWA  SASA  DR. SLAA   NA  MPENZI  WAKE  W ANAWEZA  KUOANA..!!!

Tuesday, May 21, 2013

Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay Ajiunga Rasmi na Chadema kwa kishindo


 The heavy weight MC Proj Jay, aka Dady, Joseph Haule akipokea Kadi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu Muda mfupi uliopita Mjini Dodoma Mara baada ya kujiunga rasmi na Chadema
Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA. Profesa amekabidhiwa kadi ya uanachama wa CHADEMA na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu
Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema John Mnyika(kulia)akiteta jambo na mbunge wa mbeya mjini-Chadema Joseph Mbilinyi aka Sugu muda mfupi baada ya Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay kujiunga na chadema leo Mjini Dodoma
--
Leo msanii maarufu hapa Bongo Profesa Jay (Joseph Haule) amejiunga na Chama Cha Demokrasi na Maendeleo huko Dodoma na amekabidhiwa kadi ya chama cha CHADEMA rasmi na Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi aka Sugu huko Dodoma.

Wednesday, April 17, 2013

CCM yaendelea kupasua anga Ifakara - Morogoro


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifungua Shina la Wakereketwa  wa CCM la tawi la Manjechanga, Ifakara mkoani Morogoro, Aprili 17, 2013.

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akivishwa skafu na chipukizi alipowasili  eneo la kivuko cha Kilombero tayari kuanza ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama hicho katika Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro,Kinana alikuwa akitokea wilayani Ulanga.
 Katibu Mkuu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa na watoto waliokuwa sehemu ya watu walioshuhudia  uzinduzi wa Tawi la CCM la Manjecha  eneo la Mahutanga, wilayani Kilombero.
 Katibu Mkuu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipandisha bendera kuzindua rasmi Tawi la CCM la Manjecha  eneo la Mahutanga, wilayani Kilombero
 Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Julius Mogela akionyesha kadi yake, kwa wananchi kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) baada ya kutangaza kuhamia CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Aprili 17, 2013, kwenye stebdi ya mabasi, Ifakara mkoani Morogoro
Ranfred Majiji ambaye alikuwa mfuasi wa Chadema akikabidhiwa kadi ya CCM na Kinana
 Anna Mwakitosi aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Anna Mwakitosi akishangiliwa na wafuasi wa CCM baada ya kujiunga CCM
 Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Ifarakara Mjini

Sehemu ya umati wa wananchi uliofika kwenye mkutano huo
 Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Elias Masala (kulia), akijibu maswali mbele ya Kinana jinsi alivyopanga mikakati ya kuwaletea mandeleo wananchi wa wilaya hiyo.
.Baadhi ya wafuasi wa Chadema wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara kwenye Stendi ya mabasi ya Ifakara mkoani Morogoro, Aprili 16, 2013.
Baadhi ya wafanyabiashara walilazimika kusitisha shughuli zao kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara kwenye stenbdi ya mabasi, Ifakara mkoani Morogoro. Pichani ni wauza ndizi wakiwa kwenye mkutano huo, Aprili 16, 2013.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga ngoma wakati wa uzinduzi wa Shina la Wakereketwa  wa CCM la tawi la Manjechanga, Ifakara mkoani Morogoro, Aprili 16, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akimkabidhi ubani mtoto wa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilombero, marehemu Oswald Mkokochela, Edward wakati uongozi wa chama hicho ulipokwenda jana  kuifariji familia kwa msiba wa uliotokea juzi. Ifakara Mjini,
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocenti Kalogaries akimkabidhi ubani Edward.Picha na Richard Mwaikenda na Bashir Nkromo
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...