---
DAR ES SALAAM
Vurugu
kubwa zimetokea mchana huu katika maeneo yanayozunguka eneo la Kariakoo
na kusababisha hofu kubwa na Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya
machozi na kutawanya mikusanyiko ya watu waliokuwa wamejiandaa
kuandaamana kuelekea katika Ikulu ya Magogoni jijini.
Maduka
yote katika maeneo hayo yamefungwa na shughuli mbalimbali zimesimama
pamoja na Ofisi mbalimbali zimefungwa kutokana na hofu kubwa iliyotanda.
Kwa
mujibu wa matangazo ya moja kwa moja ya Redio One wananchi wanakimbizana
hovyo kukimbia mabomu ya machozi yaliyokuwa yakipigwa na Polisi
kuwatawanya waumini waliokuwa wakitoka msikitini.
Hata
hivyo taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, waumini hao wameweza
kutawanywa na hali bado tete huku magari ya jeshi la Polisi yakielekea
katika maeneo ya Kinondoni ambapo kunadaiwa kuwa hali si shwari na
vurugu kama hizo zinaendelea.
Na
habari zilizotufikia sasa hivi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
limepeleka vikosi vyake katika maeneo ya Kariakoo ambapo vurugu zimekuwa
kubwa ili kutuliza hali ya uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment