Jengo
la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini
Dar es salaam linavyoonekana kwa nje baada ya kukamilika. Jengo hilo
linalomilikiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
lipo Makutano ya Barabara za Shaaban Robert na Garden Jijini Dar es
Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M.
Haule (kushoto) akimkaribisha Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb.), Makamu
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Mhe.
Azzan akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya NUU na Menejimenti ya Wizara
ya Mambo ya Nje. Kulia ni Balozi Rajab Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje.
Katibu
Mkuu, Bw. Haule akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Julius Nyerere walipokitembelea hivi karibuni.
Wajumbe
wa Kamati ya NUU na Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani)
wakati akiwakaribisha.
Katibu
Mkuu, Bw. Haule akitoa maelezo kuhusu Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Julius Nyerere kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama waliotembelea kituo hicho
No comments:
Post a Comment