Picha
mbali mbali za tukio la kupigwa kwa bomu nyumbani kwa katibu wa bakwata
mkoa wa Arusha Abdul Kareem Jonjo (Pichani akiwa Hospitalini) na baadhi
ya vongozi wa ulinzi na usalama mkoa wa Arusha wakionngozwa na mkuu wa
mkoa wa Arusha wakiwa kwenye matukio mbali mbali nyumbani na hospitalini
jijini Arusha leo baada ya tukio la kupigwa kwa bomu kwa katibu huyo
nyumbani kwake eneo la mtaa wa kanisani kata ya Sokon 1 jijini
Arusha.(picha na zote na Mahmoud Ahmad).
Mahmoud Ahmad Arusha
Kaimu
kamanda wa jeshi la polisi Zuberi Mwombeji ameelezea tukio la
kushambuliwa kwa bomu kwa katibu wa Bakwata mkoa wa Arusha na kusema
kuwa mnamo tarehe 25 mwezi huu muda wa saa 6:30 usiku katika mtaa wa
kanisani kata ya sokoni one iliyopo halmashauri ya jiji la arusha, mtu mmoja
aliyejulikana kwa jina la abdulkarimu idd jonjo (52) katibu wa bakwata
mkoa wa arusha na ni mkazi wa sokoni one alijeruhiwa kwa mlipuko katika vidole
vyake vitatu vya mkono wa kulia pamoja na kidevuni
Tukio hilo lilitokea chumbani kwake katika nyumba aliyopanga ambayo
inamilikiwa na Japhet S Urio. taarifa za awali zinaeleza kwamba, ndugu
Abdulkarimu Idd akiwa usingizini ghafla alishtushwa na sauti ya kishindo
kilichotokea dirishani na mara baada ya kuamka aliona kitu kikining’inia
dirishani na alipokigusa ghafla ulitokea mlipuko ambao ulimjeruhi katika maeneo
ya mwili wake yaliyotajwa hapo juu.
Kufuatia tukio hilo, aliomba msaada kwa majirani ambao walimpeleka
hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya matibabu ambapo mpaka hivi sasa amelazwa
katika hospitali hiyo na anaendelea vizuri.
Kaimu kamanda alisema kuwa mara baada ya jeshi la polisi kupata
taarifa hiyo baadhi ya askari walikwenda katika eneo la tukio na katika
uchunguzi wa awali walibaini kwamba mlipuko huo ulianzia ndani ya chumba hicho
na kutokea nje usawa wa sakafu na ukuta, pia kumetokea uharibifu wa vioo vya
dirisha moja na vipande vyake kuangukia nje na pia madumu mawili ya lita 10
yaliyokuwa na maji yalipasuka kwenye vitako vyake na maji hayo kutapakaa katika
chumba hicho.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa jeshi hilo alisema kuwa mpaka hivi
sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na jeshi la polisi
mkoani humo linaendelea na upelelezi wa kina ili kuweza kubaini chanzo, sababu
za kutokea kwa tukio hilo na hatimaye kuwakamata wale wote waliohusika na tukio
hilo.
No comments:
Post a Comment