Uharibifu uliofanwa na kimbunga Sandy New York City
Kazi ya usafi sambamba na uokozi inaendelea katika majiji mbalimbali Marekani
Jiji la New jersey lilivyoharibiwa
Nyumba zaidi ya mia moja zimewaka moto ukiachilia mbali magari na mali nyingine
Wananchi wakiangalia mabaki ya nyumba zao
Barabara zote za chini zimejaa maji
Mtoto akiokolewa maeneo ya Manhattan, New York
Njia za reli na barabara sikiwa zimeharibiwa vibaya
Watu wakiendelea kuokolewa New York
Jiji la Toronto linavyoonekana leo
Nyumba bado zimezungukwa na maji Grassy Sound kaskazini mwa Wildwood, New York
Boti iliyojikuta katikati ya njia za reli baada ya kimbunga Sandy
New York Financial District
Yadi ya magari ikiwa imefunikw ana maji
Kazi ya usafi imeanza.
Vifo
vinavyoendelea kuripotiwa kufuatia kimbunga Sandy kilichoikumba miji ya Pwani
ya MAshariki ya Marekani vinaendelea kuripotiwa. Moto uliozuka baada ya
kimbunga hicho umeunguza nyumba takribani 100 katika eneo la Breezy Point
Queens. Milipuko na kukatika kwa nyaya za umeme zimeacha eneo ya Manhattan
(eneo ambapo Al Queda walilipua majengo pacha) lilikuwa bila umeme kwa asilimia
90. Barabara za chini ya ardhi za New York ambazo husafirisha mamilioni ya watu
zimejaa maji na haijulikani ni lini zitafunguliwa.
Ajali katika
maeneo mbalimbali zime sababisha vifo vya watu 40 hadi sasa kuanzia Marekani
hadi Canada. Watoto wawili wa kiume Little wa kati ya miaka 11 na 13 walikufa
baada ya nyumba yao kuangukiwa na mti mkubwa Salem New York. Askari mmoja
aliyekuwa likizo lakini akajitosa kuwaokoa watoto hao naye alikufa ndani ya
nyumba hiyo baada ya kuwaokoa watu wengine pamoja na mtoto wa miezi 15.
Rais Obama
ameidhinisha mfuko wa maafa wa kitaifa kusaidia katika kujenga upya miundombinu
ya miji ya New York na New Jersey Obama alisema “All of us have been shocked by
the force of mother nature,” said the president, who plans to visit New Jersey
on Wednesday. He promised “all available resources” for recovery efforts.
Waokoaji
wameendelea kutafuta watu walionusurika katika mkasa huo katika miji ya Atantic
na kwingineko. RAis Obama aliongena na Magavana 20 na Mameya wa miji
iliyoathirika kwa simu na Ikulu ya White House imesema itafanya tathmini ya
uharibifu uliotokea pamoja na Mr. Christie wa Republican ambaye amekuwa
akimtuhumu Rais Obama kwa kutofanya vizuri katika kukabiliana na janga la
kimbunga hicho.
TAfsiri na: Richard Bahati
No comments:
Post a Comment