Baada ya kushindwa kwenda Kariakoo nilirudi Mwenge na kukuta watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Marafiki zangu wa dini mbalimbali tulikaa na kujadili yaliyojiri maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar na sote tulishangaa. "Hivi hasa haya maandamano ya leo yana mantiki gani kwetu Watanzania kwa ujumla?" alilalamika rafiki yangu ambaye sipendi kumtaja hapa. Nilipomuuliza ni kwa nini wao wamekuwa na utulivu wakati wengine wanaandamana, basi mjadala wa amani uliendelea kwa takribani saa nzima. Rafiki mmoja alisema hakukuwa na taarifa hizo hapa na hata kama zingekuwepo kulikuwa hakunasababu ya maana kuandamana kama ni kwa ajili ya wale walikamatwa, tulishapewa taarifa na mwanasheria wetu kuwa dhamana yake inashughulikiwa. Na kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri mtuhumiwa anaweza kunyimwa dhamana walao kwa siku 14 kisheria. Na kwamba mwanasheri wetu anashughulika na jambo hilo. Hivyo kuandamana tena inakuwa haileti maana na ndiyo maana wao hawakuwa na taarifa na legitimacy ya maandamano hayo isingekuwepo. Hata hivyo mchangiaji mwingine alisema kama hadi tarehe 01/11 hatakuwa ameachiwa kwa dhamana au kufikishwa mahakamani ili aweze kupata haki zake kulingana na katiba, then watakuwa na haki ya kuandamana kwa amani ili kumtetea kwani atakuwa anaonewa kwa mujibu wa sheria za nchi. Niliona mawazo yale ni mazuri na ningetamani wengine tuwe na uelewa wa namna hiyo kwani "haba na haba hujaza kibaba". Mimi nimeshindwa leo kufanya shopping kwa ajili ya shughuli zangu. Ina maana nimeshapoteza kile ambacho leo ningekipata kwa ajili ya familia yangu. Wengine hawakufanya biashara kabisa maeeneo ya kariakoo. nao riziki yao ya leo imeyeyuka. Je kulikuwa na sababu ya kufanya maandamano leo? Je ni upande upi unaenda kinyume na mwenzake? Na vyombo vya usuluhishi vimeshindwa kutatua matatizo ya Jumuiya ya Kiislamu na Bakwata? Pengine huu ungekuwa mjadala wenye tija. Nikiwa Kidondoni wamama walikuwa wakilalamika. Mwingine anasema jamani mimi mwanangu wa kwanza wa kumzaa ni mkristo kwani nilizaa na mkristo."mtatufanya tugombane na mabinamu? mashemeji? wakwe? watoto? waume? wake? watoto? Kwani taifa hili tunachanganyika na kuoana bila kujali kuta za kiimani. Leo hii tunaanza kuingiza chokochoko ambazo zitatufanya tusielewane"
Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo
tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari
wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu.
Askari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) wakimwingiza katika gari
muumini wa Kiislamu aliyekamatwa katika viunga vya maeneo ya Ikuu
Safari ya kuelekea Kituo Kikuu ilianza
Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leo
Askari wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu
waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la
Kariakoo
Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki
Mitaa ya Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na Askari wa Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mitaa ya Kariakoo leo
Wanajeshi wakivinjari katika mitaa ya Kariakoo leo
Ulinzi uliimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mitaa ya Kariakoo leo
Magari ya
Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika doria katika barabara
yaMsimbazi ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu
waliotaka
kuandamana.Picha zote na Happiness Mnale
No comments:
Post a Comment