ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Sunday, October 21, 2012

Nani amewabebesha mama zetu hivi vigogo jamani?

 
Mama Obama akishangiliwa na mabango yenye heshima na salama

 
Mabango yaliyotumika jana kumshangilia Sophia Simba ambayo ni mzigo na hatari, vizito hadi vinawekwa kichwani jamani..?
   WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa UWT wakishangilia bbaada ya kutangazwa jina la Mwenyekiti mpya wa Umoja huo Mhe. Sophia Simba na Makamu wake Asha Bakari katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma  usiku wa kuamkia leo (vibox na vipande vya mbao vizito vimetumika kushangilia)
 
Mabango yaliyotumika kumshangilia na kumkubali Michele Obama
 
   MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akitoa nasaha zake kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma na kumchangua Mwenyekiti Mpya Sophia Simba
   MWENYEKITI wa UWT Mhe. Sophia Simba na Makamu wake Mwenyekiti Mhe.Asha Bakari Khamis, wakiwa na furaha baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa umoja huo uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha mpiango dodoma
  VIONGOZI wa meza kuu wakishangilia baada ya kuitolewa matokeo ya kura za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa UWT, baada ya uchaguzi kufanyika kuwachagua Viongozi hao.
  Mwenyekiti mpya wa UWT Sophia Simba akipongezwa na mke wa Rais wa Zanzibar mama Mwanamwema Shein baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi wa UWT  usiku wa kuamkia leo
 
Pamoja na kumpongeza mama Simba kwa ushindi uliokuwa na ushindani mkubwa, ni wakati sasa kwa waandaaji wa shughuli hizi kwenda na wakati na kuangalia n mabango gani yanatumika katika kushangilia (chearing) na kuonyesha wagomeba wanatoka wapi. Picha za aina hii husambaa duniani kote kwa muda wa sekunde tu na si ajabu tukawa judged kutokana na taswira kama hizi. Nimeshawishika kuweka contrast ya mkutano wa marekani aliokuwa akihutubia mama Obama hivi mwezi uliopita. Wameprint vipeperushi vya plastic vizuri visivyokuwa na hatari wala mziko na mwonekano wake ni mzuri.
Jamani mnaosema mnakipenda chama, hata mabango kama hayo mnashindwa kutengeneza?
Je ikitokea fujo kama kule Mara si vigogo hivi vinaweza kuwatoa ngeu mama zetu? Next time wekezeni kwenye shughuli kubwa kama hii na nipeni tenda niwaandalie mabango mazuri tena kwa bei rahizi kabisa.   

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...