NYAMA AMBAYO IMESHAFUNGWA TAYARI KWA KUUZWA
Shirika la chakula nchini Sweden, limetoa onyo barani
Ulaya baada ya nyama iliyouzwa kama nyama nya ng'ombe kugunduliwa kuwa
nyama ya nguruwe.
Nyama hiyo inaarifiwa ilikuwa imepakwa rangi ya nyama ya ng'ombe kwa kutumia sindano.Nyama hiyo iligunduliwa na muuza duka mmoja (Svensk Cater) bada ya mteja mmoja kurejesha nyama aliyokuwa ameinunua kutoka dukani mwake akisema kuwa ilikuwa na unyevuunyevu mwingi.
Kuna hofu kuwa nyama hiyo bandia inaweza kuwa na madhara makubwa kwa afya ya watu.
Rangi ambayo ilikuwa imepakwa nyama hiyo pia inaweza kusababisha madhara makubwa. Haijulikani ikiwa nyama hiyo ambayo ilitoka Hungary imeuzwa kwa kiwango kikubwa katika maduka na mikahawa.
CHANZO CHA HABARI HII NI BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment