Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Luteni Kanali
Mussa Mrisho Mtengwa nyumbani kwa marehemu kijijini Kiwangwa, wilayani
Bagamoyo jana wakati Rais Kikwete alipokwenda kushiriki mazishi ya
Marehemu.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu
Luteni Kanali Mussa Mrisho Mtengwa wakati wa mazishi yaliyofanyika
nyumbani kwa marehemu kijiji cha Kiwangwa wilaya ya Bagamoyo mkoani
Pwani leo jioni.
Enzi
za Uhai wake Marehemu Luteni Kanali Mtengwa aliwahi kuwa mpambe wa Rais
wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi,kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka
1995.Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika Wizara ya Sheria na
kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya jeshi.
Marehemu
alifariki juzi tarehe 25 Oktoba nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar
es Salaam baada ya kuugua kwa muda na ameacha mjane watoto wanne na
wajukuu watatu(picha na Freddy Maro).
No comments:
Post a Comment