ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Sunday, October 14, 2012

Rais wa Mauritania anusurika kifo

Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, anapelekwa Ufaransa kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa alipopigwa risasi.
Rais wa Mauritania
Kabla ya kuondoka kuelekea Paris, Rais Abdel Aziz alisema kwenye hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni kutoka hospitali, kwamba ameshafanyiwa upasuaji ambao ulifanikiwa.
Wakuu walisema rais alijeruhiwa wakati wanajeshi wa serikali waliokuwa kwenye doria, walipofyatulia risasi msafara wa rais.
Inaarifiwa kuwa maafisa wawili wa jeshi wamekamatwa.
Jenerali Abdel Aziz, ambaye anaonekana na mataifa ya magharibi kuwa anasimama dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu katika eneo hilo, alichaguliwa mwaka wa 2009, mwaka mmoja baada ya kupindua serikali.

Source: www.bbc.co.uk/swahili

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...