Kikao cha bunge chaanza Dodoma na Spika wa Bunge akiingia ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
Spika Anne Makinda akiahirisha kikao cha Bunge kufuatia kuwepo kwa mahudhurio madogo ya Wabunge.
Muonekano wa siti za Waheshimiwa Wabunge mjini Dodoma leo zikionekana kuwa wazi.
Na.Mwandishi wetu Dodoma.
Kikao
cha Bunge kimeanza leo mjini Dodoma huku mawaziri wakpigwa maswali
makali na wabunge waliohudhuria kwa idadi ndogo ukilinganisha na vikao
vingine vya Bunge.
Wabunge
walianza kuuliza maswali wabunge katika wizara za Tamisemi, Fedha,Maji,
Nishati na Madini, ofisi ya rais katika kitengo cha Mkurabita na
hatimaye walimalizia katika wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Spika alimpongeza waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe
kwa kuanza kwa huduma ya safari ya Treni maalumu kwa wakazi wa jiji la
Dar es Salaam.
Baadaye
Spika alihairisha kikao cha bunge baada ya kuwepo kwa mahudhurio madogo
ya wabunge mara baada ya waziri wa Fedha na Masuala ya Uchumi
kuwasilisha bungeni Azimio la Kuridhia Marekebisho ya pili ya mkataba
wa Ushirikiano kati ya nchi za Ulaya na nchi za Afrika.
No comments:
Post a Comment