Shirika la kimataifa la kutetea
haki za kibinaadamu, Human Rights Watch, limeishutumu Syria kuwa inazidi
kutumia mabomu chane, yaani cluster bombs, dhidi ya raia.
Vibomu vidogo vidogo vinakuwa kwenye bomu kubwa
Bomu na vibomu vyake ambavyo havijalipuka
Bomu likeshaachiliwa hulipua vile vibomu vidodo vidogo na husambaa eneo kubwa sana
Syria inavyoonekana leo baada ya mabomu ya Cluster kuanza kutumiwa na Serikali dhidi ya raiya
Mlipuko wa Cluster Bomb
Majeruhi wa Cluster bomb: Momu hili lina uwezo wa kumchana chana mtu vipande vipande
Akizungumza jana, mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa wa Human Rights Watch, Philippe Bolopion, alisema inaonesha kuwa serikali haiwatii maanani kabisa wananchi wa Syria.
"Kwa muda tumekuwa tukishuku kuwa serikali ya Syria inatumia mabomu ya chane (yaani cluster bomb) lakini sasa tuna video na mashahidi kwamba serikali imetupa mabomu kama hayo kwenye maeneo ya makaazi kwa kutumia helikopta.
Kwa mfano imerusha mabomu hayo baina ya shule mbili.
Kwa hivo tunaamini kuwa serikali ya Syria inafaa kuacha haraka kutumia silaha za hatari zisokubalika kama hizi na isafishe maeneo yote ambako mabomu hayo yamemwagwa, na piya iwaarifu wakaazi wahusika juu ya hatari ya vibomu vidogo vilivotawanyika".
Source: http://www.bbc.co.uk/swahili
No comments:
Post a Comment