Mamia ya watu wanaukimbia mji wa
Bani Walid, ulioko kaskazini-magharibi mwa Libya, huku wapiganaji wa
serikali wanaendelea kutumia mizinga na kusonga mbele dhidi ya ngome ya
zamani ya Gaddafi.
Wengine walionekana wakitembea kwa miguu.
Watu zaidi ya 20 walikufa kwenye mapigano mjini Bani Walid hapo jana.
Wapiganaji wa serikali wanasema wameazimia kuwatimua wafuasi wa Gaddafi kutoka mji huo.
No comments:
Post a Comment