Waziri wa
Afrika Mashariki akishuhudia upandishwaji wa bendera ya Umoja wa Mataifa
ikiwa ni ishara ya kusheherekea miaka 67 ya Umoja huo katika viwanja
vya Karimjee jijini Dar leo.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Meja Jenerali Raphael Muhuga aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Tanzania
katika sherehe za maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu
kuzaliwa kwake.
Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta akiwasili katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es Salaam leo katika Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Umoja
wa Mataifa Tanzania kusheherekea miaka 67 tangu uanzishwe.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Dkt. Alberic Kacou akimlaki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mh. Samwel Sitta kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaa leo.
Pichani Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (katikati) akimtambulisha
Mh. Samwel Sitta kwa baadhi ya Wakurugenzi wa Mashirika mbalimbali ya
Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Waziri wa Afrika Mashariki
Mh. Samuel Sitta akipokea heshima ya wimbo wa Taifa baada ya kuwasili
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo kuhudhuria kilele
cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa baada ya kutimiza miaka 67
ya UN tangu kuanzishwa.
Mh. Samuel Sitta akikagua gwaride maalum katika kilele cha wiki ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Dkt. Alberic Kacou, Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mh. Samwel Sitta na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meha
Jenerali Raphael Muhuga wakiwa Meza kuu.
Pichani Juu na Chini ni viongozi wa
Madhehebu ya Dini nchini wakiomba Dua kwa ajili ya kubariki sherehe za
kutimiza miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Samwel Sitta akizungumza katika sherehe za kutimiza miaka 67
tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es Salaam, Sitta aliipongeza Umoja wa Mataifa kwa kuisaidia
Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ili kutokomeza
umaskini.Waziri Sitta alisisitiza kwamba bado Umoja wa Mataifa
unakabiliwa na changamoto nchini kama vile amani na usalama, tatizo la
njaa, mabadiliko ya tabia nchi na uwepo wa silaha za maangamizi.Mh.
Sitta alifafanua katika kilele cha sherehe hizo umuhimu wa kupitia na
kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo ya millennia.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Dkt. Alberic Kacou akitoa nasaha zake wakati wa maadhimisho ya
umoja huo katika viwanja vya Karimjee alisema matatizo ya njaa, kupanda
kwa bei za mafuta na mtikisiko wa uchumi duniani ni kati ya changamoto
kubwa ambazo Umoja wa Mataifa inakabiliana navyo katika dunia ya leo.
Dtk Kacou pia aliipongeza Tanzania katika juhudi zake za kupunguza vifo
vya wakinamama wakati wa kujifungua na watoto ili waweze kufikia malengo
ya millennia itakapofika 2015.Mratibu Mkazi wa UN alisema Tanzania
imepunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi.
Katibu wa UNA Tanzania Fancy Nkuhi akizungumza kwenye hafla hiyo alisema umoja wa mataifa
imefanya kazi kubwa katika kuwaunganisha vijana wa bara la Afrika.
Nkuhi alisema kupitia YUNA walitoa elimu ya afya ya uzazi na ugonjwa wa
Ukimwi kwa vijana katika mikoa kumi hapa nchini Tanzania katika harakati
ya kuelimisha vijana madhara ya ugonjwa huo na afya ya uzazi kwa
vijana.
Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa
kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium Schools) ambao walikuwa
kivutio wakati wa maadhimisho ya miaka 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa
nchini Tanzania wakiwa katika gwaride maalum kupamba sherehe hiyo.
Meza kuu ikifurahia jambo wakati wa
gwaride la watoto wa shule ya Heritage baada ya kuonyesha mbwembwe
katika kupamba sherehe hiyo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Azania wakitoa burudani ya Wimbo maalum wa kuipongeza UN kutimiza miaka 67 ya kuzaliwa.
Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa
kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium Schools) wakiimba wimbo
maalum uliobeba ujumbe wa kuhimiza utunzaji wa amani miongoni mwa
mataifa wakati wa maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya
Mabalozi, Wakurugenzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Wafanyakazi wa
UN na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo.
Pichani ni baadhi ya maafisa wa Jeshi waliohudhuria sherehe hizo.
Waziri Sitta akiwa ameambatana na
Mwenyeji wake Mratibu Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou (kushoto)
wakisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Kitengo cha maafa UN Bw.
Mdathiru Abubakar (wa pili kushoto) akielezea namna ya shirika la Umoja
wa Mataifa linavyoshiriki pindi inapotokea maafa nchini. Kulia ni Judith
Bihondwa wa UNICEF.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa
Tanzania Hoyce Temu (kulia) akifafanua utendaji wa kazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake 21 yanavyofanya kazi kwa ukaribu
na Serikali ya Tanzania kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mh. Samuel Sitta (wa pili kushoto) aliyeambata na Mratibu Mkazi wa Umoja
wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou.
Mwenyekiti wa Shirikisho la vijana la
Umoja wa Mataifa nchini (YUNA) Bw. Lwidiko Edward akisalimiana na Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta kwenye banda la
maonyesho la Umoja wa Mataifa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Waziri Sitta katika banda la maonyesho
la shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR). Katikati ni Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na kushoto ni Afisa
Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Stella
Vuzo.
Afisa Itifaki na Uhusiano wa Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) Bw. Rodney Thadeus akimweleza
Waziri Sitta jinsi ya kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)
kinavyojipambanua kwa kupokea wageni mbalimbali wanaofanya mikutano
katika kituo hicho na kutmia mwanya huo kutangaza Utalii na vivutio vya
nchi.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mh. Samwel Sitta na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt.
Alberic Kacou katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye banda la maonyesho katika wiki
ya Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment