Taarifa zilizotufikia hivi punde
zinaeleza kwamba kuna vurugu kubwa Mbagala, jijini Dar es Salaam zenye
mtazamo wa kidini, ambapo makanisa matatu yanadaiwa kuchomwa moto

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakikizingira Kituo cha Polisi cha Maturubai kilichopo Mbagala jijini Dar leo.
Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Ally Ramadhani ambaye ni dereva wa
daladala naye akiwa ameambulia kipigo baada ya kujichanganya na
waandamanaji.
Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Paul Martin ambaye alidai alikuwa akienda sokoni ndipo akaambulia kipigo.
Kibao cha kanisa kikiwa kimevunjwa.
---
WATU
wanaodaiwa kuwa ni Waislamu wamevamia makanisa mbalimbali yaliyopo
Mbagala Kizuiani jijini, Dar wakihamasisha vurugu wakimtuhumu mtoto
Emmanuel Josephat kuwa amekojolea kitabu cha dini hiyo (Msaafu) Oktoba
10, mwaka huu.
Baadhi ya makanisa yaliyoshambuliwa ikiwa ni pamoja na kuchomwa moto magari yao ni Kanisa la Sabato, Aglikana na T.AG .
(PICHA/HABARI: ERICK EVARIST/GPL)
Baadhi ya makanisa yaliyoshambuliwa ikiwa ni pamoja na kuchomwa moto magari yao ni Kanisa la Sabato, Aglikana na T.AG .
(PICHA/HABARI: ERICK EVARIST/GPL)
Wacha waue watu wote tuone wao watabaki na nani... Huwezi kumpenda Mungu
usiyemuona ukamuua na kumchukia binadamu unayeishi naye huo ni unafiki,
chuki na ubinafsi. Dunia inashuhudia mataifa yanayojiita ya kidini
yakiwa yanapigana na tena vita ya wenyewe kwa wenyewe pamoja na kuwa ni
dini moja. Upo wapi upendo Mungu yupi tunamwamini?? Unachoma makanisa na
kuua watu kwasababu ya udini, chuki na ubinafsi. Inasikitisha sana
Tanzania ya leo badala ya kukabili umaskini, maradhi na ujinga,
tunakabili DINI tena tuliyoletewa na wazungu na waarabu?
Leo utaua mkristo, kesho utaua mpagani na kwakuwa umezoea kuua keshokutwa utamuua mwislam mwenzio kwakuwa umezoea kuua na wakristo vivyohivyo. Tunashuhudia hayo somalia, afghanistan, tunisia, mali, libya, iraq na nyinginezo.
Tujaribu kubadilika, tutumie dini kuweka mahusiano yetu na mwenyezi Mungu maana hakuna liyewahi kupata manufaa kwa kumchukia mtu, wanaoeneza chuki za dini kwa kigezo cha wao na sisi eti au elimu na kuzidiana hakujengi taifa. Tafakari maisha ya vizazi vyetu vijavyo wataishi taifa lipi la watu wasioelewana??
Nawasilisha,
mzalendo.
cosmasalex@yahoo.com

No comments:
Post a Comment