Wajumbe
wa Baraza la Wawakilishi (CCM) wamelaani vikali vitendo vinavyoendelea
kufanywa na jumuiya ya mwamsho kwa kuvunja amani, utulivu na
kusababisha vurugu katika mji wa Zanzibar kuanzia jana.
Hapo jana kundi la mwamsho lilivamia nyumba za watu, maduka na kupora bidhaa kadhaa katika maduka na kusababisha hasara kubwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari huko Mbweni kwenye ukumbi wa baraza la
wawakilishi, Mhe. Hamza Hassan Juma kwa niaba ya wawakilishi wa CCM
amesema wakati umefika kwa serikali kuchukuwa hatua zinazofaa kabla
hali haijawa mbaya zaidi, kwani kuendelea kukaa kimya kwa serikali
kutatoa sura mbaya kwa wananchi.
Amesema
serikali imeunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kuondoa kasoro
zilizokuwepo na kuwafanya wananchi kuishi kwa amani na usalama na
kuweza kuondoa tofauti zao za kisiasa.
Amesema
isifike wakati Zanzibar ikawa kama zile nchi zenye machafuko na
kuwafanya wananchi wake kushindwa kuishi kwa amani na salama.
Hivyo
wajumbe hao wameitaka serikali mara moja kuwachukulia hatua wale wote
ambao wamehusika na ghasia hizo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment