kikao cha NEC kimepitisha jina la Ndugu. Phillip Mangula Kuwa mgombea wa
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara
kikao cha NEC kimepitisha jina la Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Shein nae mapendekezwa kuendelea kutetea nafasi hiyo
kikao cha NEC kimepitisha kwa kishindo jina la
Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti CCM
Taifa.
Nape Nnauye
,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na waandishi wa habari
katika ukumbi wa Kizota Usiku wa Leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na Chipukizi wa
CCM alipowasili Makao Makuu ya CCM Dodoma jana
Rais jakaya Kikwete akifungua rasmi kikao cha kamati kuu leo Dodoma.
Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha
Halmashauri kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo.Wengine katika picha
kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William
Mkapa,Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) Dkt.Ali Mohamed
Shein,Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Katibu Mkuu wa CCM
Dkt.Wilson Mukama na kulia ni Makamu mwenyekiti CCM Bara Ndugu Pius
Msekwa.Ajenda kuu ya kikao hicho ni maandalizi ya mkutano Mkuu wa CCM
utakaoanza kesho
Mwenyekiti
wa CCM Taifa,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa
Halmshauri Kuu ya CCM Taifa mjini Usiku wa kuamkia leo Dodoma
Wajumbe
wa halmashauri kuu ya CCM Taifa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa
Halmshauri hiyo uliofanyika katika ukumbi wa White House leo usiku mjini
Dodoma.
Nape Nnauye ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akipiga gitaa kwa
ustadi kabla ya ufunguzi wa kikao cha Kamati Kuu na NEC,jana Dodoma
katika Makao Makuu ya Chama.
---
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CHAMA CHA MAPINDUZI CCM iliyokaa kikao
chake jana tarehe 10 November 2012, imependekeza Ndugu. Phillip Mangula
kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara huku Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Shein , akipendekeza kuwa mgombea wa nafasi ya
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.
Nape Nnauye
,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na waandishi wa habari
katika ukumbi wa Kizota,amesema majina hayo yatapigiwa kura na wajumbe
wa mkutano mkuu siku ya jumanne.Hata hivyo ndugu Nape, amewaambia
waandishi wa habari kuwa kikao cha NEC kimepitisha kwa kishindo jina la
Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti CCM
Taifa.
Pia kikao cha NEC kimefanya Mabadiliko
kidogo ambapo leo wajumbe wa NEC nafasi kumi bara,na kumi Zanzibar
watapigiwa kura leo tarehe 11 Novemba badala ya kesho, na matokeo
yatatangazwa mara baada ya uchaguzi kumalizika.Wajumbe wote wa mkutano
kutoka mikoa yote wameshawasili.
Wakati huo huo
Rais Jakaya Kikwete kabla ya kufungua mkutano mkuu ataweka jiwe la
msingi la Makao Makuu mapya ya CCM eneo la Makulu.
No comments:
Post a Comment