Polisi
sasa wanachunguza kuhusu kifo chake cha afisa mmoja wa Usalama wa Taifa
nchini Marekani aliyejiua, afisa huyo aliyepewa jukumu la kumlinda Rais
Barack Obama.
Kwa
mujibu wa kituo cha televisheni CNN, afisa huyo aliyetambuliwa kwa jina
la Rafael Prieto alikuwa akichunguzwa kwa kutokumuarifu mwajiri wake,
juu ya mahusiano yake na mwanamke mmoja wa Kimexico.
Kwa
mujibu wa kanuni za kazi, taarifa zote kama hizo hupaswa kuripotiwa
ofisini, katika kuhakikisha kwamba usalama wa taifa haungii hatarini.
Kabla ya kujiua Prieto alikuwa ametumikia Idara ya Usalama wa Taifa ya
Marekani kwa miaka 20.
No comments:
Post a Comment