
- Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzo Mhe. Eng. Gerson Lwenge akitoa maelezo ya ramani Ujenzi wa Barabara Ndundu Somanga kwa Mh. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kipande
cha barabara ambacho ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami kati
ya Ndundu mkoani Pwani na Somanga mkoani Lindi chenye urefu wa kilometa
60 sasa umepangwa kukamilika kabla ya mwezi Juni 2013. Taarifa hiyo
imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mhe. Eng. Gerson Lwenge
wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete alipotembelea mradi huo akitokea mkoani Lindi.
Mheshimiwa
Lwenge alimjulisha Rais Kikwete kuwa, baada ya mkandarasi huyo
kushindwa kuikamilisha kazi hiyo mwezi Januari 2011 kwa mujibu wa
mkataba, taratibu kadhaa zilifuatwa ili kuhakikisha kuwa mkandarasi huyo
anachukuliwa hatua stahiki kwa lengo la kuhakikisha anaikamilisha
kilometa 28 zilizobaki kama ilivyokusudiwa.
“Hatua
kadhaa zimekwishachukuliwa ambapo kwa sasa mkandarasi ameweza kuongeza
uwezo kwa kuzalisha kilometa 5 za lami kwa mwezi na hivyo kurudisha
matumaini kuwa ndani ya miezi sita kazi hiyo inaweza kuwa imekamilika”
alisema Naibu Waziri Injinia Lwenge..
Mheshimiwa
Rais aliitaka Wizara ya Ujenzi kupitia Tanroads kuhakikisha kuwa
inausimamia mradi huo kwa karibu zaidi ili kuondoa visingizio vingine
vyoyote vinayvyoweza kusababisha mradi huo kuchelewa zaidi.
Ujenzi
wa sehemu hiyo ya barabara ambayo ndiyo pekee iliyobaki katika barabara
kuu inayounganisha mikoa ya Kusini na Jiji la Dar es Salaam, ulianza
mwaka 2008 ukiwa umepangwa kukamilika ndani ya miaka mitatu. Mkadarasi
aliyeshinda zabuni hiyo ni Kampuni ya M/S M.A. Kharafi & Sons kutoka
Kuwait kwa gharama ya Shs. 58.8 bilioni. Fedha hizo zimetolewa na
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na mifuko ya maendeleo ya KUWAIT
na OPEC.
Baada ya ziara hiyo Mheshimiwa Rais alirejea Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment