ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Sunday, December 9, 2012

ENEAGRAM SEHEMU YA NNE: ROMANTIC



Baada ya mapumziko ya weekend na sherehe za uhuru leo ni jumatatu nyingine, ambapo tunaendelea na kuichambua mada yetu ya Eneagram.
Leo tutaiongelea namba 4 (ROMANTIC)
Romantic ni mtu aliye makini sana na mwenye hisi kali sana. Huwa mara nyingi anajisikia kutoeleweka na wenzake. Ni mtu mpweke kwa kuwa anajihisi tofauti na watu wengine. Huishiwa kulaumiwa kwa sababu ya kuwa makini kupita kiasi na kukuza sana hisia zake.
Kinachoendelea ndani yake ni shauku/tamaa ya maunganiko ya maono na uhusiano wa ndani na uhusiano wa nje na wenzake. Inakuwa vigumu kwake kukubali na kuendelea kufurahia mahusiano aliyonayo kwa sababu ya mazoea yake ya kutaka  asicho nacho na kupuuzia alichonacho. Utafiti juu ya muunganiko wa maono umekuwa naye maisha yake yote. Ukosefu wa muunganiko wa maono umemweka mwenye huzuni na majonzi.  Wakati mwingi anashangaa ni kwanini watu wengine katika maisha yao wana mahusiano mazuri na maisha yenye furaha zaidi kuliko yeye. Anayo hisia ya pekee kwa upande wa uzuri. Anapitia ulimwengu uliojawa na hisia tele. Romantic anareflect na namba 2 na namba 1. Udhaifu wake mkubwa ni UVIVU.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...