ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, December 5, 2012

ENEAGRAM SEHEMU YA PILI: GIVER/MTOAJI

 
Natumaini tunaoendelea kufuatilia mtiririko huu tumeshaona kwenye utangulizi maana halisi ya Eneagram. Kama Wewe ndiyo unaona hii article leo basi fuatilia older posts ili uweze kwenda sambamba na wale ambao wamekuwa wakifuatilia mad ahii toka mwazo. Katika mduara wetu, leo tuko namba mbili (2) Mtu wa namna hii anaitwa Giver/mtoaji
Tabia za Giver/Mtoaji;
Ni mtu mwepesi sana kuhisi hisia za watu wengine. Mtu wa tabia hii anaweza kuona wanachohitaji wenzake hata kama hawafahamu. Mara nyingi huchoka sana kutambua/kufahamu mahitaji ya watu wengine hasa maumivu yao. Kwa kuwa ni vigumu kuwatimizia wote mhitaji yao basi ni rahisi yeye kujitoa. Wakati mwingine anatamani kuwa na uwezo wa kusema hapana. Nuvu zake nginyi huishia katika kuwafiniria na kuwatunza wengine kuliko jinsi anavyojituza mwenyewe. Anaumia sana kihisia pale anapoamini kuwa yeye anasaidia tu lakini wengine wanamwona kama anajipendekeza au anawavuta kwake au anawatawala kiujanja au anajifanya wakati kiukweli yeye anawasaidia tu kutoka moyoni. Anapenda wakati wote kuonekana mwenye moyo mwema, Mkarimu.....Lakini pale watu wanaposhindwa kumwelewa na kumhukumu kivingine anakasirika sana, anahangaika sana. Mwishowe anakuwa na hasira sana hivyo inaleta mgongano wa kimaslahi na wenzake katika mahali anapoishi au anapofanyia kazi.
Mathalani wewe ni mfanyakazi tu wa kawaida halafu wewe ni giver/mtoaji; unajaribu kujitolea kwa moyo wote kwa wenzako hasa wenye matatizo kama msiba, ugonjwa n.k lakini ikatokea wengine wanakuona kama unajifanya tu huna lolote; unajipendekeza tu labda kwa bosi ambaye amepatwa na matatizo, wengine wanaona kama unajifanya ii upandishwe tu cheo, kumbe wewe ni namba 2 (giver) na hujitambui. Hii ni nafasi yako ya kujitambua kwamba uko kama ulivyo si kwa sababu unajifanya, ila ndivyo ulivyo. 
Point of weakness (udhaifu wa namba 2 giver ) ni hasira. Pale unapoona kiukweli wewe unafanya yote toka moyoni halafu wengine wanakusodoa basi unakuwa na hasira na kukata tamaa. Eneagram itakusaidia usikate tamaa na itawasaidia wenzako kukutambua wewe ni namba gani na wakuhandle vipi. kwa bahati mbaya, jirani yako kitabia kama ukiangalia lile jedwali pale juu ni namba moja (perfectionist) yeye pia ana misuguano mingi na jamii. Jirani kwa upande mwingine ni namba 3 (achiever) yeye pia udhaifu wake ni mwongo mwongo. Ukiangalia mishale inakoelekea basi utaona mahali pa kuchota nguvu ni namba nne (romantic) na namber 8 (Leader) Hata hivyo kama nilivyoahidi, mwishoni nitachambua ni kwa nini namba 2 anapata nguvu kwa namba 8 na wakikaa pamoja hawatasumbuana. Wakati namba 1 na namba 8 hawawezi kukaa katika chungu kimoja.
Fuatilia kesho ambapo tutaongelea tabia namba 3 (achiever) mwenye udhaifu wa kuwa mwongo mwongo.
NB; nawashukuru wale wanaoendelea kunipa changamoto zao, wananipigia simu wanaorekebisha kiswahili changu... mengi ya haya nayatafsiri kutoka katika kiingereza kigumu kidogo hivyo nitaendelea kushukuru kwa michango na mawazo yenu)
Na mdau wako: Richard Bahati

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...