ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, December 10, 2012

ENEAGRAM SEHEMU YA TANO:OBSERVER


Kwa wale wanaofuatilia makala hii tangu mwanzo, wanaelewa maana ya neno Eneagram, lakini kwa faida ya wasomaji wapya nitatoa maana kwa ufupi kabisa kabla ya kuendelea na hatua ya nafasi ya tano.
Eneagram ni chombo cha Saikolojia  ambacho kinahusika na kujifunza zaidi juu ya Tabia za watu. Lengo kuu la Eneagram ni kutusaidia sisi binadamu kujifahamu na kuwafahamu wengine ambao tunaishi nao kila siku. Ukeshajifahamu na kumfahamu jirani yako, utaepusha migongano isiyokuwa ya lazimaa.

 Sasa tuendelee na hatua ana nafasi ya tano leo ambayo ni  OBSERVER/ MCHUNGUZI / MDADISI
Huyu ni mtu anayeweza kuelezewa kama mkimya na mchunguzi. Ni mtu anayehitaji muda mwingi peke yake kuliko watu wengine.  Mara nyingi anapenda kujitenga na wengine akiangalia kinachoendelea kuliko kushiriki matukio. Hapendi kusikiliza matakwa ya wengine, wala hapendi kutoa mapendekezo yake, maono yake wala hisia zake. Ni mtu anayejua hisia zake yeye peke yake pasi kuwa  au kushirikisha watu wengine. Ni mtu anayependa kufurahia mambo ya maisha yake yaliyopita. Anapenda kurudia matokeo yake baadaye zaidi kuliko wakati yanatokea. Mfano, mtu wa namna hii atakuwa anaangalia achievements zake za masomo, maisha kumbukumbu mbalimbali na atazifurahia sana na atatumia muda mwingi sana kuangalia na kufurahia matokeo hayo. Kukaa peke yake haimchoshi kwa sababu maisha yake kiakili ni mepesi na machangamfu. Kwa ke ni muhimu zaidi kutunza wakati wake kwa nguvu yake hivyo kuishi maisha rahisi yasiyo na ugumu ili awe mtu wa kujitosheleza iwezekanavyo.
Udhaifu wake ni; huyu ni mtu ambaye ni lazima afahamu kila kitu kinachotokea, na hatoi mapendekezo zaidi tu ya kutaka kufahamu. Ni mtu ambaye hakuna habari itakayompita,hasa taarifa za habari na magazeti na blogs kila kitu atataka akijue, shida tu ni kwamba kujua hivyo vyote kunaifurahisha tu nafsi yake na wala sio kwa faida ya jamii inayomzunguka.
Na mdau wenu;
Richard Bahati

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...