Muuaji Adam lanza ambaye ameelezewa kuwa na na utaalamu wa hali ya juu wa kulenga shabaha. Lanza alikuwa na miaka 20 tu na ndani ya dakika 3 alikuwa ameshauwa watu 26 na yeye kujiua mwenyewe
Adam akifanya mazoezi ya kulenga shabaha na vidole vyake
Mama wa Adam Lanza ambaye aliuwawa kwanza na mwanaye kabla hajaenda shuleni kupukutisha watoto na waalimu wao
Waombolezaji wakisali katika kanisa katoliki la Mt Rosa wa Lima kuombea marehemu wao.
Roby Parker akijaribu kuzuia machozi baba mzazi wa Emillie aliyeuwawa na na Adam Lanza
Emillie enzi za uhai wake
Mary Sherlack aliyekuwa na umri wa miaka 56alikuwa mwalimu wa Saikolojia shuleni hapo kwa miaka mingi. Alimkimbilia muuaji kumzuia asidhuru watoto ndipo alipojikuta naye anauwawa. May alikuwa anastaafu baadaye mwaka huu.
Rais Obama ameshindwa kujizuia wakati akitoa hotuba yake kufuatia kuuwawa kwa watoto 20 na waalimu wao.
Obama akilia wakati akongea na waandishi wa habari si tu kama rais lakini pia kama mzazi mwenye watoto
Noah Pozner huyu nikati ya watoto 20 waliopigwa risasi na kufa
Paroko wa St Rose de Lima Parish aliwa kwenye mshtuko mkubwa
Wazazi wakilia kwa uchungu baada ya kukuta mtoto wao kauwawa.
Watoto wakiondolewa katika eneo la hatari
Polisi wamefika eneo la tukio wakati tayari muuaji alishamaliza kazi yake
Utawatuliza na nini wazazi hawa?
Mtoto akimshukuru Mungu kwa kupona na janga la Adam Lanza
Watoto wakiwa hawaamini kama wamepona
No comments:
Post a Comment