
Waandamanaji wakipambana na polisi

Waandamanaji wakirusha mabomu ya petroli
waandamanaji wakizunguka viunga vya Ikulu Jiji ni Cairo
Waandamanaji wakipambana na polisi
Polisi wakiwa tayari kukabiliana na waandamanaji
Mwandamanaji akijiandaa kurusha bomu la machozi
Ukuta uliokuwa ukizuia waandamanaji kuingia ikulu ambapo hata hivyo ulivunjwa na waandamanaji
Makabiliano ya uso kwa uso na polisi
Wafuasi na wapinzani wa Rais Morsi wakitwangana
Waandamanaji wakichoma moto magari na malinyingine
Makabiliano yamezuka
kati ya wafuasi wa Rais wa Misri Mohammed Morsi na wapinzani wake nje ya
ikulu ya rais mjini Cairo.
Wafuasi wa rais huyo wameharibu mahema
yaliyowekwa nje ya ikulu hiyo na wapinzani wa Morsi walioanza kukesha
nje ya ikulu hiyo Jumanne kupinga mamlaka aliyojilimbikizia.Makamu wa rais Mahmoud Mekky,amesema kuwa mabadiliko yaliyofanyiwa katiba hiyo yanaweza kukubalika na upinzani.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Hillary Clinton amesema mazungumzo yanahitajika haraka kuhusu katiba hiyo.
Maelfu ya wapinzani wa rais wameapa kuendelea na maandamano yao nje ya ikulu ya rais mjini Cairo.
Baadhi wameweka mahema nje ya ikulu na sasa wanuzunguka ukuta wa ikulu hiyo.
Maelfu wameizingira ikulu wakimpinga rais kwa kujilimbikizia mamlaka
Wakati mmoja polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao ambao walikuwa wamevuka ukuta wa seng'enge.
Vikosi vya usalama vilitoa taarifa vikisema kuwa rais Morsi ameondoka katika ikulu hiyo na ameomba utulivu.
Waandamanaji hao wanapinga hatua ya rais kujilimbikizia madaraka mapya na kusababisha kuundwa kwa rasimu ya Katiba.
No comments:
Post a Comment