ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, December 14, 2012

Rais wa Zanzibar Dr Ali Shein Azindua Sensa Ya Miti


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipima urfu wa mti alioupima urefu kwa kutumia chombo maalum cha kupimia miti,wakati wa uzinduzi wa zoezi la sensaya miti (woody Biomass Survey) katika hifadhi ya Taifa ya msitu wa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kwa pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bibi Arna Klepsivik,wakata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa sensa ya miti (woody Biomass Survey) katika hifadhi ya Taifa ya msitu wa Jozani jana
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipima mti kujua upana wake baada ya kuzindua zoezi la sensa ya miti (woody Biomass Survey) katika hifadhi ya Taifa ya msitu wa Jozani jana,(kulia) Naibu waziri wa Kilimo na Maliasili Mtumwa Kheir Mbaraka na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Maliasili Affani Othman Maalim,(kulia).Picha na Ramadhan Othman Ikulu-Zanzibar
--
WIZARA ya Kilimo na Maliasili na Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu, Baraza la Mainispaa Zanzibar, Mabaraza ya miji Pemba na Hamlashauri zote za Wilaya zimetakiwa kushirikiana katika kuimarisha mazingira kwa kupanda miti katika barabara za mijini na vijijini kwa Unguja na Pemba.
Kauli hiyom imetolewa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa sensa ya miti Zanzibar, hafla iliyofanyika huko Jozani Mkoa wa Kusini Unguja. Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa Srikali iko tayari kutoa msukumo na kuhakikisha kwamba lengo hilo linafanikiwa kwa wakati na kusisitiza haja ya kutunzwa na kudumisha miti hiyo. Alisema kuwa sensa ya miti ni muhimus ana katika kupanga mipango ya maendeleo na kueleza kuwa kukamilika kwa kazi hiyo kutawezesha kupatikana takwimu muhimu na kuelewa wingi, ubora na aina za miti ya misitu, viungo na matunda iliyopo Zanzibar.
“Tunahitaji kuwa na takwimu sahihi za sasa ili tuweze kupanga mikakati bora na mipango mikakati bora na mipango muhimu ya maendeleo, hasa katika kuidhibiti misitu na miti iliyopo na kujipanga katika kuongeza mingine”, alisema Dk. Shein. Aidha, Dk. Shein alisema kuwa zoezi hilo litahusisha miti ya misitu, matunda na biashara ikiwemo karafuu hivyo, kukamilika kwa kazi ya sensa ya miti itawezesha kuzifahamu takwimu muhimu za zao hilo ikiwemo wingi, umri, urefu wa mikarafuu na maeneo yenye mikarafuu. Dk. Shein alitoa changamoto kwa Wizara ya Kilimo na Maliasili kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko zitumie matokeo ya utafiti wa upimaji wa miti ili kuyaondosha matatizo yaliopo na hatimae Zanzibar iweze kurudi katika biashara yake ya kuuza matunda nje ya nchi hasa Dubai kama ilivyokuwa hapo kabla. 
 
  Alisema kuwa takwimu zitakazotokana na kazi hii ya sensa ya miti ni muhimu na zitasaidia pia, katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni agenda muhimu kitaifa na kimataifa. Alisisistiza kuwa umuhimu huo unaonekana hasa katika nchi za visiwa kama Zanzibar ambapo kama hatua za mapema hazikuchukuliwa athrai kubwa kwa jamii kiuchumi na kimazingira zinaweza kutokeza. Dk. Shein alirejea wito wake wa kuwataka wananchi wasikate miti ovyo ikiwemo minazi na miti mengine ya matunda na misitu.  
 
Pamoja na hayo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kwa kutoa shukurani maalumu kwa washirika wa maendeleo ikiwemo Serikali ya Norway kupitia Ubalozi wake uliopo nchini kwa kuunga mkono na kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kat

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...