ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, December 1, 2012

"TOA DAKIKA MOJA KWA UKIMWI"


 



Mdau akimfariji mgonjwa wa ukimwi

Mdau Richard akimfanyia massage mgonjwa wa ukimwi


mdau Rchard akimsikiliza mwathirika wa ukimwi aliyekimbiwa na ndugu zake wote

Mdau richard Akimtuliza mgonjwa mwenye hasira na kukata tamaa baada ya kunyanyapaliwa na ndugu zake

Mdau Richard akimwandaa mgonjwa wa Ukimwi aliyekuwa katika hatua ya mwisho ya kukata roho

pamoja na wadau wengine wachache tulishiriki mazishi ya mwathirika aliyekimbiwa na ndugu wote, tulikuwa chini ya watu 6 tu tulisaidiwa na Halmashauri ya Jiji la Lusaka. Hakuna ndugu hata mmoja aliyeonekana.

 

 Tanzania Bila Maambukizi Mapya, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi Inawezekana”

 
Wadau nimekumbuka project hii niliyoifanya huko Zambia miaka michache iliyopita. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuweka bayana jinsi wagonjwa wa Ukimwi wanavyojisikia pindi wanaponyanyapaliwa. Katika Slide show hiyo utaona wengine wamediriki kusema kuwa hata Mungu hayupo. Sisi tulio wazima tumejijengea tabia hii ya kuwanyanyapaa wagonjwa wa Ukimwi kiasi kwamba tunawaona kama nusu binadamu. Ikumbukwe kwemba, familia zetu nyingi zimefikwa na mahasibu haya. Kama sio mwana, mkeo, mumeo, mjukuu, mjomba, baba mkubwa, baba mdogo, mama mkubwa, mama mdogo, shangazi, binamu, mkwe, mpwa basi ni wewe mwenyewe. Hakuna atakayeweza kusimama na kusema kuwa hajawahi kukutana au kufiwa na ndugu wa karibu kutokana na janga la Ukimwi. Ni wangapi tunaendagamahospitalini kuwatembelea wagonjwa hawa? Tuwatembelee hata kama hatuna pesa za kuwanunulia juice. Tuwasaidie hata kufua mashuka yao.Tuwapatie massage. Tuongee nao. Mara kwa mara ninapotembelea wagonjwa hawa, ninakutana na walokole wakiwaombea. Sio mbaya kumwombea mgonjwa. Ina kilichonikera ni pale unakuta mtu anamwombea mgonjwa na kumwambia "YESU ANAKUPENDA" na sisi tunakupenda lakini mgonjwa amezungukwa na inzi kwa kuwa amejisaidia kitandani. Hakuna mlokole anayesema ngoja kwanza tumbadilishe papmas au mashuka, tumwondolee kinyesi au mkojo, tumwogeshe, tumlishe japo kipande cha chungwa halafu tumwombee. Ukifanya hiyo ndugu yangu hata maombi yako yatafika na mgonjwa anapona japo kwa siku hiyo. Nawatia moyo twende kuwatembelea wagonjwa hawa. Wamejaa Mwananyamala, Lugalo, Ilala, Muhimbili. Tena tuwazoeshe hata watoto wetu kuwa na matendo ya huruma kwa wagonjwa hawa. Hiyo ndiyo thawabu. Sio maneno tu. Kwa atakayependa anitafute nimpe semina ya namna ya kuwahudumia wagonjwa wa ukimwi bila kuathirika. Namba yangu ni 0716391060, tena unaweza kunitumia email nikakutumia pacage yote ya namna ya kuishi pamoja na mjonjwa aliye mahututi bila kupatwa na maambukizi. Nitaweza pia kukupatia video ya hizo clips hapo juu ya namna nilivyoshitiki kwa matendo, kuuguza, kufariji, kutunza na hata kumwandaa mgonjwa na kifo pale kifo kinapokuwa hakiepukiki tena.
Hata hivyo, msisitizo wa maambukizi mapya nionavyo mimi umepungua sana. Hebu nenda kwenye kumbi za starehe usiku uone jinsi vijana wanavoishi katika dunia yao "isiyokuwa na ukimwi" Ufuska wa kila aina baada ya kunywa na kuvuta kila aina ya tumbaku. Uvaaji wa kila aina unaoleta vishawishi vya kila aina. Tanzania bado hatujawa na uthubutu wa kuongelea mambo haya hadharani ingawa kila mtu anaona jinsi jamii inavyozidi kukumbatia kinachoitwa "mabadiliko ya tabia mtu" Wana harakati hawajaweka mkakati wa kuwafikia na kuwafundisha vijana kuhusu madhara ya ngono. Kutumia KONDOM hakutoshi hata kama zingekuwa zinasaidia. Hivi mlevi na kondom wapi na wapi. Mapenzi ya jinsia moja yanazidi kushika kasi na bado hatujawa tayari kuyazungumzia hadharani. Inabidi yazungumzike maana maana maambukizi yake ni rahisi zaidi. Vijana wengi wa leo hawana elimu ya Ukimwi. Kama ni kubashiri basi kama ilivyobashiriwa kuwa miaka hii tunayoishi sasa itakuwa na yatima wengi sana na ndivyo ilivyo, miaka 10 ijayo kutakuwa na upungufu mkubwa sana wa watoto kwani vijana wengi sana watakuwa wameathirika au wamekufa. Kwa hiyo reproduction cycle itakuwa hasi na hali hii itachukua muda mrefu sana kurudi kwenye mzunguko wake wa kawaida. Matokeo yake itabidi tuajiri watu kama Wachina na Wahindi kuja kujaza nafasi za kazi .........
Mwenye kuweza kutafakari jinsi ukimwi unavyoenda atashawishika kuamini kwamba ni kama program. (this is not a point of discussion though)
 Nawatakia wote siku njema ya kutafakari kuhusu ukimwi duniani. Ki ukweli hii ni tafakari ya kila siku. Maana Ukimwi tupo nao kila mahali, majumbani, maofisini, viwandani, makambini, mashuleni, vyuoni.......
Na mdau: Richard Bahati
 

 

 

 

1 comment:

  1. Hii imenigusa sana mdau. dah! watu wanateseka kweli mwanangu.
    Yatupasa kujilinda kwa hali na mali hasa sisi vijana maana kama miaka kumi ijayo kutakuwa kweli hakuna uzao kama tutaendelea kufanya ngono zembe hivi.
    Dah asante mdau kwa elimu hii

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...